UCHAGUZI wa Wabunge wa Viti Maalum umeleta sura nyingi mpya huku baadhi ya vigogo wakiwemo Maua Daftari, Alshaymaa Kweigy, Magreth Mkanga na Shyrose Bhanji wakishindwa katika uchaguzi uliofanyika jana.
Matokeo hayo yalitangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi huo, Zakhia Meghji ambaye pia ni Katibu wa uchumi na fedha.
Nafasi ya uwakilishi Viti Maalum, walemavu nafasi mbili, walioshinda
ni Stella Alex na Amina Mollel, Stella alipata kura 51 huku Amina Mollel
akipata kura 44.
Wagombea wengine ambao walishindwa katika uchaguzi huo ni Alshamaa Kweygir alipata kura 38, Khadija Taya ‘Keisha’ alipata kura 37, Magreth Mkanga kura 27, Elizabeth Msaki kura 26, Bahati Hemed kura 17, Salma Ramadhani kura 15, Hidaya Juma kura 10, Halima Seif kura tano, Sitta Kelvin kura nne, Suzan Mushi kura nne.
Wengine ni Lupui Mwaswaya kura nne, Edith Kagomba kura tatu Mary Kalumuna kura tatu, Rwehema Joshua kura tatu, Sarah Mkumbo kura tatu na Riziki Lulida kura moja.
Nafasi za uwakilishi wa wanawake kundi la NGO, nafasi mbili walioshinda ni Dk Gertrude Rwakatare na Rita Mlaki.
Rwakarate alipata kura 82 na Mlaki kura 59.
Walioshindwa katika kundi hilo ni Khadija Aboud kura 36, Maua Daftari kura 29, Zainabu Gama kura 10, Angela Mwangoza kura 10, Saum Abdallah kura tisa, Grace Mahumbuka kura tisa, Chiku Mugo kura tisa, Sitti Ally kura nane, Diana Lenatus kura saba.
Wengine ni Nebro Mwina kura saba, Angela Bayo kura nne, Renatha Kapinga
kura nne, Devotha Mtonyole kura nne, Hawa Isengwa kura tatu, Christina
Kulunge kura tatu, Said Sharifu kura tatu na Mickness Mahella kura moja.
Nafasi ya uwakilishi wa wanawake vyuo vikuu nafasi mbili walioshinda ni Dk Jasmine Tiisekwa na Ester Mmasi.
Dk Tiisekwa alipata kura 61 na Mmasi alipata kura 46.
Walioshindwa katika nafasi hiyo ni Dk. Alice Kaijage alikuwa mshindi wa tatu kwa kupata kura 39, Lucy Saleko kura 25, Theo Ntara kura 24, Maurine Castico kura 20, Juliana Manyerere kura 16, Mariam Khamis kura 12, Mary Lubeleje kura 11, Kuluthumu Makame kura 10, Godliver Kaijage kura nane.
Wengine ni Mwadawa makame Ame kura saba, Furaha Mramba kura tano, Zainabu Zonzo kura tano na Tumwangile Mwakyusa kura nne.
Kwa upande wa nafasi ubunge wanawake wafanyakazi nahasi mbili walioshinda ni Angellah Kairuki na Hawa Chakoma. Kairuki alipata kura 47 na Chakoma alipata kura 47.
Wagombea wengine katika nafasi hiyo walikuwa Shyrose Bhanji alipata kura 30, Asmayah Ally kura 29, Lamela Malya kura nane, Vedate Ligalama kura saba, Amina Mweta kura sita, Bijuma Hamad kura tano, Meck Gushaha kura nne, Janeth kabeho kura nne, Flora Masakilija kura nne.
Wengine ni Zeleikha Salim kura nne, Esther Kimwei kura tatu, Mwanamwanga Mwadunga kura mbili na Mwantumu Othuman kura mbili.
Katika nafasi ya wagombea Ubunge Viti Maalum CCM Kundi la vijana Zanzibar nafasi nne walioshinda ni Khadija Nasri Ally alishika nafasi
ya kwanza kwa kupata kura 117, Munira Mustafa Khatibu kura 105, Nadra Juma Mohamed kura 103, Time Bakari Sharifu kura 91.
Walioshindwa ni Salma Seif Ally alipata kura 87 na Mwanaenzi Hassan Suluhu kura 66.
No comments:
Post a Comment