Inaonekana
kwamba Darius Makambako 50 akiwa na mke wake Precious 45, walitaka sana kupata
mtoto, lakini daktari bingwa alikuwa amewaambia wanandoa hao kuwa mume alikuwa
TASA. Hakukuwa na shaka, wenzi hao walikuwa wamechoka kuwa katika ndoa ya miaka
23 bila mtoto.
Kwa
hiyo Makambako, askari wa Jeshi la Polisi (Idara ya Trafiki), baada ya
kushurutishwa na mkewe, aliajiri jirani yake Evans Mastano, 52, afisa mwenza wa
polisi katika jiji la kibiashara la Dar-es-Salaam kumpa ujauzito mke wake.
Kwa
kuwa Evans alikuwa tayari ameoa na ni baba wa mabinti wawili warembo, na pia
kwamba alifanana sana na Darius kindakindaki, mpango huo ulionekana kuwa mzuri
kwa wanandoa hao wa familia mbili lakini bila kumshirikisha mke wa Evans.
Makambako
alimlipa Mastano Shilingi 2,000,000 za Kitanzania kwa kazi hiyo ambayo
angeshiriki tendo la ndoa na mkewe kwa jioni tatu kwa wiki kwa miezi 10 ijayo
ya 2016.
Evans
alijaribu sana, jumla ya mara 77 kumpa ujauzito mke wa rafiki yake Precious,
lakini alishindwa kabisa kufanikiwa.
Ripoti
zinasema Precious, ambaye kikazi ni muuguzi katika zahanati ya kibinafsi
aliamua kuchukua likizo ya miezi mitatu (Machi hadi Juni 2016) ili kutenga muda
wake wa kulala na rafiki mkubwa wa mumewe na jirani ili kupata mtoto wake wa
kwanza, lakini mwanamume huyo alishindwa kumpa mimba licha ya mume kuwaacha
kitandani siku nzima mara nyingi.
Na
Precious aliposhindwa kupata ujauzito kwa miezi 10, hata hivyo, Makambako
hakuelewa na kusisitiza kwamba Evans afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu, ambao
alifanya Januari 2017.
Uchunguzi
wa daktari
Ulionyesha
kwamba Evans Mastano pia alikuwa TASA matokeo ambayo yalimshtua kila mtu
isipokuwa mkewe (Evans), ambaye alilazimika kukiri kwamba Evans hakuwa baba
halisi wa watoto wake wawili, bali walikuwa wa binamu yake, Edward.
"
_Nililazimika kulala kwa siri na Edward, binamu yake wa kwanza, kupata watoto
hawa wawili baada ya kugundua kuwa mume wangu hangeweza kunipa ujauzito kwa
miaka miwili",_ Angela aliambia _Dar-es-Salaam Today News._
Sasa
Makamboko anamshtaki Evans kwa ukiukwaji wa masharti ya mkataba katika jitihada
za kurejesha pesa zake, lakini Evans anakataa kwa sababu alisema
hakumhakikishia kupata mimba, lakini tu kwamba aliahidi kujitahidi na angefanya
juhudi za uaminifu.
*SWALI*
:
1.
Je. Makambako ana haki ya kudai arudishiwe pesa yake?
2.
Nini itakuwa hatma ya ndoa kati ya Evans na mkewe Anjela?
Chanzo:
*DAR-ES-SALAAM LEO.*
No comments:
Post a Comment