14 April, 2011

Magufuli, Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu.

Moja ya sifa katika serikali inayofuata misingi ya kidemokrasia ni kuwajibika kwa viongozi “accountability for leadership” hii ni pale inapoonekana haijaweza kutekeleza kazi zake hivyo huwajibika kwa wale inaopaswa kuwatumikia.

Wakati mwingine huwajibika ikitokea kuwepo hali ya kutaka kuongeza ufanisi. Kwa mfano, inapotokea nafasi uliyokabidhiwa inakuwa kikwazo katika kutimiza malengo uliyojiwekea kulingana na taratibu basi hatua inayofuata ni kujiuzulu nyadhifa hiyo.

Hii tunajifunza kutoka kwa Mwl. Nyerere alipojiuzulu uaziri mkuu na kumwachia kawawa alioutumikia takribani miezi sita tu baada ya kupewa wadhifa hiyo.
Kilichomfanya Mwl. Kujiuzuru ni kile kilichoitwa kuwa anataka kwenda kuimarisha chama chake cha Tanu, ambacho kwake ndilo lilikuwa ndoto yake katika utumishi wake.

Kwa tabia ya viongozi wetu ambao kwa sasa wamegeuka kuwa watawala wanamchukulia nyerere kuwa alijikoseshea ulaji, kwa sababu wao tumbo mbele maendeleo nyuma. Hawa ni wale waliopotoka, wamesahau misingi ya uwajibikaji na kukosa uzalendo. 
Ikiwa ni miezi michache ipatayo mitatu tu kwa Rais Kikwete tangu atangaze baraza lake watu wengi walitarajia mengi kutoka kwa mawazili hasa waziri wa ujenzi John Maghufuli anayeaminika kuchapa kazi kwa umakini, na kwa kujituma zaidi.

Baada ya kutangazwa kwa baraza hilo haya yalikuwa baadhi ya maoni ya wananchi waliyoyatoa katika mitandao kwa Rais kikwete kwa kumtangaza Maghufuli kama wazili wa ujenzi. Mmoja wao aliandika,
“Baraza kwa ujumla ni zuri sana, tunawatakia uwajibikaji na ufanisi mzuri katika utekelezaji wa majukumu yenu. Nimefurahishwa na Magufuli kurudi kwenye barabara. Hongera Rais, Mungu awape nguvu na hekima katika utendaji wenu siku zote”
Mwingine naye akaongezea “Hongera (rais) kwa aliyekushauri na hongera kwako pia kwa kusikiliza kwa makini na kutenda. Baraza ni zuri. Lakini ujue watu wanasema ni zuri (sana sana kwa sababu umemweka Magufuli mahali stahili), basi umlinde atachape kazi”
Haikuishia hapo huyu naye akaibuka   “ongera mzee kikwete,sasa fanya kazi, mpe nafasi zaidi mzee magufuli akufanyie kazi nzuri, … tuko nyuma yako,kuwa mkali pambana na ufisadi rudisha heshima ya ccm
Mwalimu Nyerere - Alijiuzulu Uwaziri Mkuu na kumwachia Kawawa
Ally Hassan Mwinyi- alijiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani kufuatia mauaji ya Shinyanga
Idi Simba - Alijiuzulu Uwaziri wa Viwanda na Biashara kufuatia Kamati Teule kuundwa kuhusu misamaha ya kodi ya Sukari
Kighoma Malima - Sikumbuki vizuri alijiuzulu katika mazingira yapi na kama alijiuzulu kabisa au alitishia kujiuzulu...



No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...