25 May, 2011

USWAHILI BWANA!


YANAYO TUFANYA TUWE WASWAHILI...

 1.Unamwita mtu usiyemjua(wala kukutana nae kabla)aunt au anco.
  

 2.Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copies).
  

3.Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo  siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.
  
4.Una machupa ya maji matupu ya shampoo perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.
  
5.Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali,chidi,mamu,dida n.k.
  

6.Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapo kuja  kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k.
  
7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k  ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.
  

8.Familia yako ina migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku 10 au  zaidi.
  

9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano  usiku sana )na mara nyingi huwa una beep tu.
  
10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.
  

11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko  inavyoruhusiwa.
  
12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi  asingekuwa vile yule.
13. Ualikwapo kwenye sherehe au mkutano hufika baada ya muda ulopangwa kupita waweza zidisha hata masaa mawili mbele au zaidi.
14. unapokuwa kwenye shere hutaki kuchukuliwa moving iwapo kunavideo inayotengenezwa.

2 comments:

  1. Amos C. Belege: likes this.

    ReplyDelete
  2. Christopher Haule: dats true jose hizo 14 behaviour tunazosana wabongo mi na wewe lazima kuna kama si chini ya 3 zinatuhusu kubali au kataa

    ReplyDelete

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...