21 December, 2011

ONGEZEKO LA POSHO ZA WABUNGE

Wakati wananchi wa kawaida Tanzania wakiwa wanaendelea kulalamikia kupanda kwa gharama za maisha; Wabunge wa Bunge tukufu la Tanzania wanachekelea kupandishwa kwa posho kutoka Tsh. 70,000/=  mpaka Tsh. 200,000/=  wanayolipwa sasa!

Baadhi ya wana harakati nchini wamesha anza mapambano kwa kufanya maandamano kupinga kwa ongezeko la posho hizo. Jana Arusha ilifanya maandamano huku wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali wakionyesha dhahiri kukerwa, kuchukizwa na kulaani kitendo hicho. 

Wengi walihoji kwa kusema iweje posho iongezeke wabunge tu? Vipi kuhusu makundi mengine? Ina maana ni wabunge pekee maisha yamepanda??!! Wamesahau wananchi vijijini ambao bado wanakunywa maji machafu ya kwenye visima? Huku wakifia njiani wakipelekwa hospitali kutokana na miundo mbinu mibovu ikiwemo barabara na mawasiliano!? Wamesahau wanafunzi wanakaa kwenye vumbi kwa uhaba wa madawati? Huku waalimu wao wakiwa na malimbikizo ya mishahara kwa muda mrefu?!

Matatizo hayo na mengine lukuki wameyafumbia macho huku wakiona kwao ni sahihi kwa ongezeko la posho hizo. Bila shaka hawakumbuki wapo bungeni kuwakilisha wananchi wa majimbo yao. Wamesahau walipokua wakiomba kura kwa kuwapigia magoti wananchi.

Si sawa, si sawa hata kidogo. Mimi (jojo) naungana na wale wote wanaolaani na kupinga ongezeko la posho za wabunge.

Nitakubaliana na posho hizo endapo tu wafanya kazi wengine wote wakiwamo Waalimu, Madaktari na makundi mengine kuongezewa posho. Pia nitakubaliana na posho hizo endapo ukali wa maisha utapungua ikiwemo kushuka kwa gharama za petroli, vyakula. Pia nitakuwa radhi kwa posho hizo nikiona miundo mbinu madhubuti kama barabara na madaraja. Vifaa na madawa hospitalini, na mashuleni kuwepo na waalimu wa kutosha na vifaa vya kufundishia. Hatuoni aibu kwa Taifa la Tanzania kuwa na wahitimu wa shule za msingi ambao hawajui kusoma wala kuandika. Ah jamani! Hii ni aibu kubwa

TANZANIA BILA ONGEZEKO LA POSHO ZA WABUNGE INAWEZEKANA

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...