24 December, 2011

WACHAGA TUMERUDI KUHESABIWA


Asikwambie mtu, nyumbani raha bwana! Wahenga wanasema nyumbani ni nyumbani na wachaga kamwe hawaachi asili yao ya kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka kujumuika na familia zao Moshi. Kitu cha machalari (ndizi nyama) na pembeni unashushia na mbege! Weeeeee!! Wacha kabisa.

Pamoja na shida ya usafiri inayokuwepo kila inapofika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, kama vile nauli kupanda bei, nafasi kujaa kutokana na idadi kubwa ya wasafiri hasa kwa safari za kanda ya Kaskazini
(Moshi na Arusha) lakini bado wana kwetu tuna hakikisha hatukosi kwenda kuhesabiwa. Mimi pia ni miongoni mwao, natarajia kuondoka kesho alfajiri saa 11. Dar es Salaam nitapa miss, naamini kutabaki na utulivu hasa kwasababu pilika zitapungua.

Kwa moyo mkunjufu na upendo, napenda kuchukua fursa hii kuwatakia wasomaji wangu wote wa blog hii Heri ya Krismas na Mwaka Mpya. Chonde chonde, ulevi NOMA! Usiendeshe gari ukiwa umelewa, kumbuka kutumia kinga. Taifa bado linakuhitaji. Nawapenda sana.



1 comment:

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...