21 December, 2011

POLENI NDUGU ZETU KWA MAAFA YA MAFURIKO


Jiji la Dar es Salaam limezizima kwa maafa ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha tokea jana. Kwa taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa wametangaza kwamba mvua zinaweza kuendelea mpaka tarehe 23 Mwezi huu! Hali ni tete kwa makazi, wakazi kwa baadhi ya maeneo ya Jijini Dar es Salaam.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi kwa mvua hizi ni pamoja na Tandale kwa Mtogole, Kigogo, Jangwani, Msasani, Temeke, Mburahati, na sehemu zilizopo mabondeni.
Watu wanaoishi mabondeni wameshauriwa wahame mara moja ili kunusuru maisha yao.
Mpaka sasa taarifa za kuaminika imeripotiwa kwamba watu 8 wamepoteza maisha, na mmoja kati ya hao alinaswa kwa nyaya za umeme huku uharibifu mkubwa wa mali za watu kuharibiwa vibaya kutokana na mvua hizi zinazoendelea kunyesha!
Poleni sana ndugu zetu mlioathiriwa kwa namna moja au nyingine kutokana na mvua hizi! Watanzania wote tupo pamoja katika kipindi hichi kigumu. Msife moyo.
Hata hivyo serikali imetenga maeneo maalum kwa waathirika ikiwemo shule ya Msingi Kibasila na huduma zote ikiwemo chakula, dawa, magodoro na mablanketi kupewa waathirika hao.Huku kazi ya uokoaji ikiendelea maeneo mbalimbali.
Nitaendelea kuwapa taarifa kadiri zitakavyo patikana.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...