Valentine's Day ni siku muhimu ambayo inakupasa usheherekee katika hali ya kipekee zaidi. Mwaka huu
siku ya wapendanao itaangukia siku ya Jumanne, kwa kawaida hi ni siku ya kazi lakini haitazuia upekee na umaalum wa siku hii.
Zawadi, Kutembeleana, Salamu ni miongoni mwa muhimili wa siku hii. Ikumbukwe kwamba Valentine's
Day si kwa ajili ya Mpenzi wako tu! Unaweza kuonyesha hisia zako kwa ndugu, wazazi, walezi, jamaa na
marafiki zako.
- Zawadi ndogo huweza kuwa na maana kubwa sana!
- Na kama una uwezo wa zawadi kubwa, hii ni siku nzuri zaidi kumzawadia yule unaemkusudia
- Mishtukizo ( Suprises) huleta msisimko zaidi!
- Kupata mlo maalumu wa pamoja. Itapendeza zaidi kama utaandaa chakula hicho mwenyewe
- Haijalishi kama ni mlo wa mchana (lunch) au mlo wa usiku (dinner). Ni vema ukaandaa mwenyewe
- Pendeza! Nukia! siku hiyo iwe ya mvuto zaidi, onekana tofauti na siku nyingine
- Mazingira ya nyumba/ Chumba yawe safi, na mvuto wa pekee
- Haijalishi unafanya nini? Ila jinsi unavyofanya!
- Pata mawazo mapya, kuboresha mawasiliano/ mahusiano
- Kutoka pamoja
NB: Karibu na uongeze mawazo hapa ya nini cha kufanya siku ya Valentine's
Nawatakia siku kuu njema, bila mwaka huu Valentine's Day itakua ya tofauti na pekee kuliko nyingine zote zilizowahi kutokea kabla.
Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wasomaji wa blogi yangu kwamba nawapenda sana, na nitaendelea kuwaletea mambo mazuri ili mzidi kuelimika na kuburudika.





No comments:
Post a Comment