Haya ni matokeo ya Tiba ya Babu Ambi
sola anayotumia nyumbani kwake.
“Hatuwezi
kupoteza muda na fedha zetu kwa kwenda kunywa dawa ambayo haitibu, hii
ni kuwarubuni wananchi, wengi wameuza mali zao, wengine kutumia akiba
ya fedha walizokuwanazo kwenda Loliondo wakijua wangepona lakini cha
kushangaza ni kwamba baadhi yetu wanakufa. “Wengine wako mahututi baada
ya kupewa kikombe, tulikuwa na matumaini ya kupona hadi tuliacha
kutumia vidonge vya kurefusha maisha vya ARV, hatuna mengi zaidi ila
tunaomba umtafute mwenyekiti wetu akueleza zaidi,” alisema mmoja wa
wanachama wa Tanopha. Mwenyekiti wa Tanopha, Julius Kaaya, aliliambia
Uwazi kwa njia ya simu kuwa taasisi yake ilipeleka watu 14 kunywa dawa
Loliondo lakini hakuna hata mmoja aliyepona. “Nakumbuka kwamba kipindi
tunaenda huko Loliondo Machi 19, mwaka huu, tulifanya mkutano na
waandishi wa habari, tulifika Samunge
Machi
22,
ambapo Machi 24 walikunywa dawa hiyo kila mmoja akiwa na matumaini ya
kupona. “Baada ya siku 20 tangu wanywe dawa hiyo walienda hospitali
kuangalia kama wamepona, daktari aliwaambia hakuna hata mmoja
aliyepona, siku 90 baadaye majibu yakawa yaleyale,“ alisema Kaaya.
MCHUNGAJI MTIKILA Naye Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation,
Christopher Mtikila kwa upande wake amesema kwamba dawa hiyo haitibu na
analishughulikia suala hilo ili kumfikisha mahakamani pamoja na
mawaziri, wabunge na viongozi wa juu waliokunywa kikombe.“Mawaziri hao wamewahamasisha wananchi kwenda Loliondo kunywa dawa, lazima tuwashitaki pamoja na viongozi wa dini waliopiga debe,” alisema Mtikila. Viongozi wa dini waliohamasisha ni Askofu Thomas Laizer na Martine Shayo. Baadhi ya Mawaziri waliopata kikombe ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli. Wengine ni wabunge Augustino Mrema, Edward Lowassa na wakuu wa mikoa Yohana Balele na Abbas Kandoro. TAMKO LA WIZARA Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda, alisema hivi karibuni kuwa kikombe cha Babu siyo tiba na kwamba wote waliokwenda Loliondo, walipoteza muda. Kauli ya waziri, ilifuatia ripoti ya uchunguzi wa madaktari bingwa kwamba kikombe cha Babu wa Loliondo, hakitibu. WABUNGE NAO Katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 10, baadhi ya wabunge walitaka Babu wa Loliondo achukuliwe hatua kwa sababu dawa yake haitibu. Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, alikwenda mbali zaidi kwa kutaka mawaziri waliokwenda Loliondo, wahojiwe na waseme kama wamepona, kwani wao kwa kiwango kikubwa walihusika kupotosha umma.
Babu akiwa amepozi nyumbani kwake.
Wanaharakati
wameeleza kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo wanamfungulia Babu Ambi,
mojawapo ni kumfilisi mali zote alizochuma endapo atakutwa na hatia ya
ulaghai, wakati wa kutangaza maono aliyopewa na Mungu kuhusu tiba ya
kikombe. Wanadai kuwa Babu Ambi, mkazi wa Kijiji cha Samunge, Loliondo,
alitumia matatizo ya Watanzania ya kuugua maradhi sugu ili
kujinufaisha, hivyo akatengeneza ulaghai wa tiba ya kikombe kwa maelezo
kwamba ni ufunuo aliopewa na Mungu. Madai hayo yanakuja wakati ambao
Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa
kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land
Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up). Babu Ambi, ameshahama nyumba
chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye
mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi
inavyomeremeta.
UTETEZI
WA BABU Kwa upande wa Babu Ambi, ameendelea kushikilia msimamo wake
kuwa dawa yake imeponyesha wengi. “Kama hawajapona siyo makosa yetu.
Tuliwaambia kabla kuwa katika tiba hii kigezo cha kwanza ni kuwa na
imani na hapa tuna uthibitisho wa kutosha wa watu walioponywa na maajabu
ya dawa hii wakiwemo wagonjwa wenye Ukimwi,” alisema Babu Ambi na
kuongeza kuwa anapigwa vita na wengi kwa sababu ya wivu. Kuhusu utajiri
wake, alisema kuwa yeye hana mamilioni ya fedha kama inavyodaiwa ila
akakiri kumiliki nyumba ya kisasa pamoja na magari mawili ambayo amesema
yanamsaidia kubeba dawa pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa
Loliondo. KUHUSU KIKOMBE Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa KKKT Arusha,
Thomas Laizer, zaidi ya watu milioni tatu wameshatibiwa Loliondo. Kila mgonjwa
alikuwa analipa shilingi 500, hivyo kwa hesabu ya watu milioni tatu,
maana yake kikombe kimeshaingiza zaidi ya shilingi bilioni 1.5.
Mjinga ni nani......



No comments:
Post a Comment