Baada
ya wawakilishi wote wa Tanzania kutolewa kwenye jumba la Big Brother Afrika,
Hilda na Julio.. imefahamika kwamba ni kura chache sana zilizomfanya mshiriki
wa Zimbabwe kubaki kwenye jumba hilo japokua nae alikua kwenye hatari ya
kutoka.
Katika
tetesi za vyanzo vikuu vya habari nchini humo, Hilda amesema “jamani najisikia
vibaya kweli, unajua ukiwa na watu wanaokupenda wanaofurahi kwamba umefika
ulipofika alafu unatolewa bila kutarajia inauma kuliko hata ungetolewa labda
ukiwa unachukiwa na mtu fulani, au mtu flani hataki niwe kwenye nyumba, hii
imekua tofauti kwa sababu mashine imeamua tutoke”
Amesema
“imefika sehemu lazima tukubali na sasa hivi kila wiki kati ya watu wanne
watakua wanatoa watu, wanne ndio anabaki na kuingia Up Ville ambapo ndio kuna
kina Prezzo huko kwa hiyo nafikiri kutakua na watu kama kumi na nne ambao
watajumuika na mastaa alafu ndio nafikiri mfumo wa kawaida ndio utaendelea japo
hatujui itakuaje”
Alipoulizwa kama kuna uhalali wa yeye kutolewa,
Hilda amesema “sidhani kama ni halali kwa sababu nafikiri mimi nilikua mmoja
kati ya wachezaji wazuri kwenye nyumba, pia naweza kusema Mzimbabwe ambae
amebaki kwenye nyumba amenipita tu kwa kura mbili, kama ningepata watanzania
wawili wanipigie kura kabla ya jana asubuhi saa kumi na mbili kuna uwezekano
tungekua wote ndani ya nyumba sasa hivi, nimepitwa na kura mbili tu yeye
alipata kura nane, mimi sita alafu wengine ndio wanafata… najua ningepata hizo
kura mbili na nyie mngekua mnakula bata sasa hivi kupitia Tv nisingewaangusha,
lakini namshukuru Mungu kwa kweli nataka niwaambie Asante sana”
No comments:
Post a Comment