Utata
kama Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani) ana mimba au la, umetatuliwa
baada ya mwanamitindo maarufu Bongo anayefahamika kwa jina moja la
Martin kutoboa siri kuwa ni kweli staa huyo ana mimba ya miezi mitatu...
Akizungumza,
Martin ambaye ni rafiki wa karibu wa Lulu anayesota rumande Segerea,
Dar akiwa mshukiwa wa kwanza wa kifo cha Steven Kanumba, alisema kwa
hesabu zake tangu msichana huyo aliponasa ni takribani miezi 3 sasa.
Lulu akiwa na mwanamitindo Martin Kadinda
WALIJARIBU KUICHOROPOA MARA KADHAA
Jamaa
huyo alifunguka kuwa baada ya Lulu kushtuka kuwa ni mjamzito alimweleza
marehemu Kanumba ambapo kwa pamoja walijaribu kuichoropoa mimba hiyo
lakini ikasema “sitaki” (ikashindikana).
Aliendelea
kudai kuwa, baada ya mpango huo kufeli waliamua kuiacha hadi Lulu
alipokumbana na dhahama ya kukaa nyuma ya nondo hadi leo.
“Yeye (Lulu) na Kanumba walijaribu mara kadhaa kuitoa lakini ikashindikana.”alisema mwanamitindo huyo.
NDIYO CHANZO CHA ‘SHESHE’ LAO
Jamaa aliweka wazi kuwa ‘sheshe’ kubwa kati ya Lulu na marehemu Kanumba lilihusiana na mimba hiyo...
“Kanumba alikuwa akitaka Lulu akatoe mzigo huo, lakini Kalulu Kadogo (Lulu) alikataa katakata,” alisema na kuongeza:
“Aisee ilikuwa ni ishu ya siri sana.”
sorce: global publishers & zehotpot
No comments:
Post a Comment