16 May, 2012

MADAKTARI WASHINDWA KUTIBU UGONJWA HUU


MADAKTARI nchini Uganda wameshindwa kutibu ugonjwa wa mguu wa tembo uonaomsumbuwa mtoto Vincent Oketch.
Vincent mwenye umri wa miaka 10 amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo uliosababisha mguu wake kuwa na uzito mkubwa kuliko uzito alionao.
Kutoka na ugonjwa huo unaomsumbua mtoto huyo, wazazi wake pamoja na madaktari nchini Uganda wameanza kutafuta msaada wa matibabu kutoka kwa madaktari nchini Uingereza.
Mmoja wa madaktari waliojitolea kumsaidia mtoto huyo kwa kushirikiana na wazazi wake ni Dk Isaac Osire ambaye ameanza kutafuta msaada kutoka kwa madaktari wa kigeni kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Vincent Oketch, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Peta nchini Uganda, anapigania maisha yake baada ya mguu wake huo kurefuka kiasi cha kumzunguka.
Vincent hakuwai kufikiria kuwa ipo siku atakuja kuishi maisha hayo wala hakufikiria kama mguu wake utaendelea kukuwa kila wakati.
Hata hivyo mtoto huyo anaendelea kuishi maisha ya tabu baada ya madaktari nchini humo kushindwa kumtibu.
Wazazi wa Vincent walianza kuangaikia matibabu yake tangu akiwa na mwaka mmoja na nusu, lakini kutoka na umaskini wao walishindwa kumpeleka katika kliniki mbalimbali kwa ajili kufanyiwa utafiti wa ugonjwa huo.
Hata hivyo, Vincent alivyozidi kukuwa ndivyo mguu wake pia, ulivyozidi kukua na kurefuka zaidi kiasi kwamba hawezi kutembea wala kujisogeza mwenyewe.
Kibaya zaidi kwa mtoto Vincent ni kwamba hawezi hata kuvaa kaptura wala suruali na badala yake amekuwa akivaa magauni ya kike na sketi, kitendo kinachomliza kila wakati, huku watoto wengine  wakimsikitikia na kutokwa machozi kutokana na umbile lake kumlazimu avae mavazi ya kike kila wakati.
"Hakika suala hilo linamsumbua sana Vincent kwa sababu anapaswa kuvaa nguo za kike na kila anapovaa anatokwa machozi, huku watoto wengine pia wakitoka machozi pindi wanapomwona”anasema baba wa Vincent Tito Opoya.
"Kweli mwanangu ni mdogo sana, lakini uzito wa mguu wake unamshinda hata yeye mwenye kuunyanyua pia, suala la yeye kuvaa nguo za kike, inamnyima raha mwanangu. "
Dk  Osire ameamua kuchukua jukumu la kutafuta namna ya kuokoa maisha ya mtoto huyo, kutoka na ugonjwa huo unaoendelea kutafuna miguu ya mtoto huyo kwa ndani ambao kwa lugha ya kigeni unaitwa ‘fasciitis’.
Dk Osire hivi sasa ameanza kuonana na madaktari kutoka nchini Uingereza ili kujaribu kumsaidia mtoto huyo.
Dr Osire, ambaye anaendesha Taasisi ya EDYAC inayosaidia kutoa matibabu ya bure kwa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharimia matibabu yao.  Alimchukuwa mtoto huyo katika gari lake na kumpeleka hospitali jijini Kampala kuangalia kama watalaamu wanaweza kumsaidia.
“Baada ya Dk Osire kumfikisha mtoto huyo hospitalini na kufanyiwa vipimo vya MRI ilibainika kwamba, Vincent alikuwa akisumbuliwa na maradhi  ambayo yanashambulia mfumo wa fahamu wa mwili na kusababisha mwili kushindwa kujiendesha wenyewe badala yake viungo vya mwili vinaanza kurefuka ikiambatana na uvimbe”anasema Dk Osire.

Dk  Osire anasema: "Madaktari wa hospitali hiyo wameshauri kuwa ingekuwa ni vyema kwa Vincent kukatwa miguu ili kumnusuru na ugonjwa huo Ila mimi ninaogopeshwa sana na uamuzi huo kwa sababu bado tunajaribu kuwatafuta watalaamu mbalimbali na bado ni vigumu kujua ukweli kuhusu ugonjwa unaomsumbua Vincent.”
Dk Osire ambaye ameamua kubeba jukumu la kuhangaikia matibabu ya Vincent baada ya kubaini kwamba wazazi wake hawana uwezo anasema, “Bado tunahitaji kuwapata watalaamu kutoka Uingereza watakaoweza kutoa ushauri juu ya suala la mtoto Vincent  kwa sababu tatizo lake haliwezi kutatuliwa na wataalaamu wa hapa nchini na ndiyo maana bado tunahangaika kupata watalaamu kutoka nje”anasema Dk Osire na kuongeza:
“Nitajitahidi kufanya chochote nitakachoweza kukifanya ili kuokoa maisha ya mtoto huyu na kumfanya aweze kupata nafasi ya kurudia maisha ya kawaida.”
Baba wa mtoto huyo Tito naye anasema, “Nina imani kuwa madaktari wanaweza kufanya jambo lolote linaloweza kumsaidia mtoto wangu na nina mshukuru Dk Osire kwa mambo yote anayofanya kwa ajili yetu.”
Dk Osire amekuwa na moyo wa kuwasaidia  watoto wenye matatizo nchini  Uganda, huku akiwachukua watoto wenye hali mbaya katika gari lake na kuwapelekea hospitali.
Katika hatua nyingine, Dk Osire anasema mbali na kuwatafuta watalaamu watakaoweza kumsaidia mtoto huyo, pia wanahitaji msaada wa fedha kwa sababu kuna watoto wengi nchini Uganda wenye matatizo mengi ya kiafya kama Vincent, lakini wanakosa huduma kwa sababu maeneo ya vijijini hakuna hata magari ya kubebea wagonjwa na kwamba wana imani kwamba watapata taasisi ama mashirika ya nje kwa ajili ya kusaidia watoto nchini Uganda.

Source: Jackson Odoyo (Japo Investment)

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...