Ndugu zangu na rafiki zangu.
Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza.
Naomba msisikitike sana.
Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri
ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu
anapompulizia pumzi ya uhai.
Hili lilipangwa hata kabla sijatokea
duniani miaka 42 iliyopita! Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu
asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo
kutokea?
Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie.
Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.
Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu.
Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.
Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza
mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na
vijijini ndani na nje ya nchi.
Nilitumia kila aina ya uwezo wangu
kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya
energy. Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania
maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?
Waziri gani aliyewafikisha mahakamni
watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za
matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya
2011.
Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini
ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope
Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali
Mungu wetu wa haki.
Waziri gani aliyefunga biashara ya
wanyamahai? Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa
watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.
Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa.
Nilitegemea vita hii, na ninaamini
tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa
makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema. Imesemwa
issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka
amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine
wamenununua magari na wengine majumba.
Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka
wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na
benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na
vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati
wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma
nilikokopa au amtafute muuzaji.
Kote huko utapata rekodi ya bei na mode
of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi
wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu
anashughulikia hilo.
Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na
dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu
utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni. Yapo mengi yasiyo
sahihi yaliyosemwa.
Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na
muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni
hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na
kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa
ni zile zilizopata chini ya alama 50.
Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye
biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni
za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya
alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa
na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.
Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa
binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana
Novemba 2010. Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama
waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya
utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug
biashara hiyo. Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala.
Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.
Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana.
Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15. Wasalaam
No comments:
Post a Comment