19 June, 2012

DAWA YA UKIMWI YAPATIKANA

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa makala mbalimbali zinazihusu maswala ya afya, magonjwa mbalimbali ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na ugonjwa unaoonekana kutopatiwa dawa kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu umeanza kuathiri watu (UKIMWI) ukiendelea kuua mamia kwa maelfu duniani utagundua kwamba kuna uwezekano mkubwa sana dawa hiyo ipo na watu walishaigundua lakini kuna uwezekano kwamba kuna watu fulani wanaizuia kwa sababu wananufaika kupitia watu kuendelea kuambukizwa gonjwa hili hatari linaloangamiza wengi hasa katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba ukimwi ulitengenezwa na watu kwa makusudi Fulani, lakini kuna madaktari wengi kutoka pande zote za dunia ambao karibu kila mwaka huwa wanakuja na matokeo Fulani baada ya kufanya tafiti kwa muda mrefu zinazoleta matumaini makubwa kwamba sasa dawa inaenda kupatikana lakini ghafla hawasikiki tena na badala yake wanaibuka wengine namna hiyo, kama ilivyotokea miaka ya hivi karibuni Israel, Marekani na hata Korea ya Kusini kuweza kugundua dawa zilizofanyiwa majaribio na nyingine zilizo tayari zikisubiri tu kujaribiwa kwenye mwili wa binadamu lakini ghafla hakuna kinachosikika tena!

Wataalamu wanasema kuweza kupata dawa hii kunahitaji pesa nyingi sana za kufanyia utafiti ikiwa ni pamoja na wataalamu wengi kushirikiana ila pesa ambayo huwa inatolewa ni kidogo na hakuna ule ushirikiano wa kutosha, ni kwa nini? Tumeshuhudua ndugu zetu wengi wakipoteza maisha, watoto yatima wakiongezeka mitaani nguvu kazi ya taifa kupotea ikiwa ni pamoja na viongozi wakubwa serikalini kwa sababu hii sasa ni kwa nini nguvu nyingi zisiongezwe katika kutafuta tiba au angalau chanjo ili kupunguza hii hali ambayo inazidi kuwa ya hatari?

Gazeti la Mwananchi la tarehe 10 Desemba ya mwaka 2011 lilitoa taarifa ya utafiti uliofanywa baina ya hospitali ya KCMC ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ushirikiano na chuo kikuu cha afya cha Duke cha nchini Marekani juu ya uwezekano wa kupatikana chanjo na tiba ya ukimwi.
Utafiti huo uliofanywa na Dk Reddy akishirikiana na wataalamu wa hapa nchini, Profesa Noel Sam, Profesa Saidi Kapiga na Sarah Chiduo, ulibaini kuwa kuna watu ambao baada ya kuambukizwa VVU miili yao imeweza kutengeneza kinga imara ambazo zimeweza kudhibiti kabisa virusi na wala hawahitaji kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo maarufu kama ARV.
Dk Reddy alisema watakachofanya kwenye utafiti wao, ambao uliwahusisha pia wanasayansi wa nje ya nchi; Profesa John Bartlelt na Profesa John Crump, ni kutengeneza chanjo ambayo itawafanya watu wote kuwa na uwezo wa kutengeneza kinga hizo. Chanjo hiyo alisema kwa upande mwingine wanategemea itakuwa ni tiba.

Alisema tafiti nyingi ambazo tayari ziko kwenye mchakato zinaweza kuzaa matunda ndani ya kipindi cha miaka saba ijayo.
Cha msingi nafikiri tujaribu kuondoa ile imani ya kwamba dawa ya ukimwi haipo wala haiwezi kupatikana na kujaribu kushinikiza utafiti zaidi na kufuatilia matokeo ya tafiti hizo na kuielimisha zaidi jamii juu ya maswala yote ya afya, athari zake na hatua zilizofikiwa hizo ni sambamba na harakati za kupunguza umaskini na majanga mengine yanayokumba jamii mbalimbali hasa katika hizi nchi maskini na zinazoendelea.

Source: View TZ

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...