MAMA wa Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu ametoa kichekesho cha mwaka
baada ya kufanya mahojiano na Tv moja ya jijini Dar akilenga kumsafisha
mwanaye kwa kuwananga marafiki na magazeti pendwa, Ijumaa lina ripoti
kamili.
Katika mahojiano hayo, Mama Wema ‘alibwabwaja’ mengi huku
akitupia lawama makundi mengine wakiwemo marafiki wa kiume wa mwanaye.
AJISIFU KUMLEA WEMA VIZURI
Bila soni wala aibu, mzazi huyo
alijisifu kumlea VIZURI Wema, jambo lililoibua maswali miongoni mwa
watazamaji wa runinga hiyo huku wengine wakiomba kamusi ya Kiswahili
sanifu ili kujua maana ya neno ‘vizuri’.
“Japo sikumnyonyesha lakini mwanangu nimemlea vizuri. Ana maadili mazuri ya Kiafrika,” alisema mama huyo.
AFUNGUKA BILA BREKI
Katika mahojiano hayo aliyoyafanya Juni 19,
mwaka huu, mama huyo aliwashushia lawama mashoga wa mwanaye akisema
walimpoteza Wema kwa kumpeleka kwa waganga wa kienyeji kipindi cha nyuma
na kumfanya awe ‘mawengemawenge’.
“Nimehangaika sana usiku na
mchana kumfanya mwanangu arudi kwenye hali yake ya kawaida. Marafiki
zake walimpoteza, walimpeleka kwa waganga kitendo ambacho kilichangia
kwa kiasi kikubwa kumpoteza mwanangu, akawa mtu asiyejielewa,”
alifunguka bila breki.
ALIKOROGA, ATALINYWA
Kwa kauli hizo tu, Ijumaa lilipokea simu
nyingi kutoka kwa mastaa na wasomaji wa kawaida wakidai kuwa mama huyo
alikuwa amewachekesha kwani tangu kipindi hicho kilipokwenda hewani siku
hiyo, marafiki wote wa Wema waliamua kujichenga na kumwachia maisha ya
peke yake huku wakidai kama anataka kuishi kwa raha atafute kisiwa cha
kuishi huko.
“Mdomo uliponza kichwa, sisi ni marafiki zake na
tunafanya naye kazi kwa upendo mkubwa lakini kwa kauli ya mama
tunaonekana tunajipendekeza. Acha aishi dunia ya peke yake,” alisema
mmoja wa waigizaji kiwango hapa Bongo.
TURUDI KWA MAMA WEMA
Akiendelea kuropoka mambo bila kuanika ushahidi wa wazi, mama huyo
alisema marafiki wote wa Wema ni wanafiki na kama mwanaye anataka
marafiki wa kweli, ni yeye mama, dada yake Wema (pengine yule anayeishi
Kumekucha- Sinza) na ndugu wengine wa karibu.
ETI WEMA MAMBO SAFI
Mama Wema alifunguka kuwa katika kipindi hiki
ambacho mwanaye mambo yake yanamwendea vizuri hataki marafiki wanafiki
wanaomfuatafuata Wema kwa lengo la kumchafua.
SNURA ACHAFUKA
Awali kabla mama Wema hajaanza kutiririka
runingani, msanii wa filamu Snura Mushi aliongea akisema yeye na Wema ni
marafiki wakubwa mpaka watu wanamsema vibaya kwamba, amekuwa mpambe wa
Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.
Snura akasema wao wanapendana
sana, watakuwa sambamba hadi siku kila mmoja atakapoishi maisha mengine.
Wema naye alikazia hapo kwa kukiri yeye na Snura ni marafiki wakubwa.
Lakini mama Wema alipopewa muda wa kuwa hewani, alimchana hadi Snura kwamba ni walewale. Hebu msikie:
“Mwanangu Wema, nakwambia mimi mama yako, jihadhari na marafiki
wanafiki. Rafiki wa kweli ni yule anayekujali, wengine wanafiki. Haohao
ndiyo wanaokucheka ukiandikwa vibaya kwenye magazeti, wewe huna rafiki
wa kweli.”
HIVI ALIJIULIZA HILI SWALI?
Kwa mujibu wa wadau wengi waliopiga
simu kwenye dawati la Ijumaa walihoji kwa nini mzazi huyo hakuanika
chanzo cha utajiri wa Wema na kumhoji mwanaye alikopata Sh. milioni 400
za kununulia nyumba (ingawa imebainika si yake) kwani hana filamu
aliyocheza ikamwingizia mkwanja huo wote.
WOLPER NAYE HAKUWA SALAMA
Katika tuhuma hizo, mama Wema
alimshambulia mwigizaji Jacqueline Wolper akidai alimkosea mwanaye
(kipindi hicho alichopotea) kwa kumwambia kuwa amchezeshe filamu moja
ili amlipe fedha ya kwenda kununua kitanda wakati yeye anaamini mwanaye
kamwe hajawahi kukumbana na tatizo la kukosa mahali pa kulala katika
maisha yake.
KITUKO
Wakati akihojiwa, mama huyo alionesha kitanda kipyaaa na
cha kisasa akidai ndicho alichokuwa akilalia Wema tangu akiwa mdogo hadi
leo ana miaka 23. Hata hivyo, kitanda hicho kilionekana kama
kimenunuliwa jana yake.
WOLPER ASHINDWA KUJIZUIA, AMJIBU MAMA WEMA
“Mh! Sijui ataelewekaje huyo mama na tena kwa bahati mbaya huwa
sitazami hizo local channel (televisheni inayotazamwa na eneo fulani
pekee) ambazo nasikia ndiyo ametumia kunizungumzia na kunishirikisha
mimi na mwanaye. Mimi huwa natazama DSTV. Niliambiwa na watu walioona.”
AORODHESHA WANAUME WA WEMA
Akitambaa na msururu wa wanaume
waliotoka kimapenzi na mwanaye (bila kujali kuwa siyo maadili kwa binti
wa Kiafrika), mama Wema alisema ni kweli mwanaye ‘amesharukaruka’ na
vijana wawili watatu.
Aliwataja marehemu Steven Kanumba
(alithibitisha alijua) kuwa alikuwa miongoni mwa wanaume wa Wema huku
akimshukuru na kumuomba Mungu amrehemu huko mbele za haki aliko.
Pia
mzazi huyo alimtaja mjasiriamali, Jumbe Yusuf Jumbe na kumalizia na
mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ kuwa hao
ndiyo wanaume wa Wema pekee.
Majina hayo siyo mageni kwani ni
yaleyale yaliyokuwa yakichorwa na magazeti pendwa ingawa alimsahau
mwanamuziki wa Mashujaa Band, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ huku Wema
mwenyewe akiomba majina ya wasanii Khaleed Mohamed ‘TID’ na Herry Samir
‘Mr Blue’ yakatwe kwenye listi.
MTITI KWA DIAMOND
Mariam alipofika kwenye jina la Diamond, ndipo
akawaka si kitoto akidai kuwa hakuwahi kumtarajia kama anaweza kuwa
mkwewe hata siku moja kwani ni mpuuzi na mhuni.
“Mtu wamekutana tu
huko, bila kushirikisha wazazi anamvalisha pete kwenye klabu za muziki.
Nilishajua mwisho wake sababu ni mhunimhuni tu aliyemtumia mwanangu kama
daraja la kupandia afike anakotaka.”
LAKINI TUJIKUMBUSHE
Wakati Wema anamtongoza Diamond kupitia
mtandao wa kijamii wa Facebook mwaka 2010, tayari ‘kichaa’ huyo wa Bongo
Fleva alikuwa juu kwani tayari alishavunja rekodi kimuziki kwa kutwaa
tuzo tatu za Kili hivyo si kweli kwamba alitaka umaarufu.
FAMILIA YA DIAMOND
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia
ya Diamond kilipenyeza habari kuwa, hawakufurahiswa na kitendo cha mama
Wema kulipuka runingani kwani hata mama Diamond naye ana uwezo wa
kufanya hivyo.
WEMA VIPI?
Baada ya kipindi hicho kwenda hewani, Wema
aliwasiliana na chumba chetu cha habari akilia na kuhaha kuwa mama yake
alikuwa amezungumza vitu ambavyo hata yeye hakutarajia (meseji zake
tunazo).
ONYO LA MAGAZETI PENDWA
Katika kipindi hicho, mama Wema
alipigilia msumari wa mwisho pale alipoyapa mwezi mmoja magazeti pendwa
yaache kumwandika mwanaye.
“Haya magazeti ya udaku (pendwa) nayapa
mwezi mmoja kuanzia leo hii ninavyoongea, yaache kumwandika mwanangu,
safari hii wajue hawadili na Wema, wanadili na mimi mama yake.
“Wewe
Shakoor wewe, Shakoor (Jongo). Si unajifanya upo karibu sana na Wema
kumbe mnafiki mkubwa, nilishawahi kukupopoa mawe, hujakoma, sasa
marufuku kwa mwandishi yeyote kuja hapa nyumbani kwangu.”
MEZANI KWA MHARIRI
Mama Wema ana uhuru wa kuzungumza kama walivyo
Watanzania wengine, ameshatoa yake ya moyoni, sasa awaachie wengine nao
ni zamu yao.
Source ( Ijumaa Newspaper)
Maoni ya JoJo The Fighter
"Nyota ya Wema ina ng'aa ndio maana anaongoza kuandikwa kwenye vyombo vya habari. Magazeti pendwa yamekua yakimuandika binti wa watu (Wema) kwa mambo mabaya tu! Kana kwamba hakuna lolote jema alilofanya. Kama ishu ni kuwa na wanaume tofauti, mbona dada zenu, watoto wenu na wanawake/ wake zenu nao wanao lakini hamuwaandiki? Iweje yeye tu!? Kweli mlitegemea mama wa watu amzungumze vibaya mwanae? Mnaujua uchungu wa mwana nyie? Kwakweli imefikia wakati wa kujirekebisha, mambo mengine ni too personal ku display hadharani. Muacheni mtoto wa watu. Mmeshamsema vya kutosha, mmeuza kupitia yeye vya kutosha."
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...

-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Baada ya miaka 13 ya kuwapo katika fani ya sanaa ya maigizo, hakuna shaka kwamba, Ste...
No comments:
Post a Comment