16 June, 2012

Kwaya ya Kwetu Pazuri yazua Gumzo nchini
















Ujio wa waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la Waadiventista Wasabato ya Rwanda ‘Ambassador of Christ’ ‘Kwetu Pazuri’ umezua gumzo baada ya waimbaji hao kupewa ulinzi wa hali ya juu ulioleta kadhia kwa wapenzi na mashabiki wa kwaya hiyo.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano unaoendela kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni, waumini hao walidai kuwa ulindwaji wa waimbaji hao na mabaunsa, unaleta karaha kwao na ni kinyume na imani ya dini hiyo inayowataka wote kuwa sawa.
Naye mmoja wa waumini hao Daniel Jonas alisema kuwa Jumamosi iliyopita walijikuta wakikosa ladha ya mikutano hiyo, hasa pale walinzi hao walipowasukuma hovyo waumini waliokuwa karibu na wanakwaya hao wakati wakipita.
“Nchi yetu ina amani, sidhani kama kuna mtu wa kutaka kuwadhuru waimbaji hao ambao ni kipenzi cha wengi hapa nchini,” alisema.
Kwaya hiyo ililijipatia umaarufu, hasa baada ya kuja nchini mara ya kwanza na kufanya maonesho makubwa na yenye mafanikio, wamekuwa wakija nchini mara kwa mara, lakini utaratibu wao wa kutumia mabaunsa umeanza kutumika awamu hii, ambapo inawakera washiriki wa dhehebu hilo na mashabiki wao, ambao kimsingi ndiyo wenyeji wa wanakwaya hao.
Habari kutoka ndani ya uongozi wa kanisa hilo, zimeeleza kuwa, vijana hao hawakuwekwa na kanisa bali ni kampuni moja inayoshughulika kusambaza kazi zao.
Mbali na hilo uongozi huo ulisema kuwa lengo la kuweka walinzi hao, ni kutaka kupunguza kero na msongamano kutoka kwa wapenzi wa kwaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...