08 June, 2012

Usafi wa CHADEMA uko wapi?

Waumbuaji wanakaribia kuumbuka!!

Evance Komu, mtoto wa Mkurugenzi wa Fedha wa CHADEMA na Mbunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA mama Anna Komu, anakabiliwa na shitaka la wizi wa fedha katika benki ya STANBIC. Fedha hizo aliziiba kwa kushirikiana na wazazi wake ambao ni vionozi wa CHADEMA kati ya 2010 na desemba 2011. Je, wizi huu si hatari kwa nchi? Mtoto wa kiongozi wa chama cha upinzani kukabiliana na kesi ya wizi wa fedha Benki! Habari kamili gazeti la Majira la tarehe 7.6.2012. Usafi wa CHADEMA uko wapi wadau?
CHADEMA kwa biashara!!!! Walichangisha watu kabla na baada ya uchaguzi na kwenye operasheni sangara,wakatoa namba za kuchangia kupitia vyombo vya habari hadi leo hawajatoa taarifa ya mapato na matumizi, sasa hivi wameibuka na mpango wao wa M4C wanawachangisha fedha tena watanzania tena masikini waliosema wana maisha magumu na kuitaka serikali kuwaboreshea maisha yao!
MCHUMBA WA DK.SLAA APIGWA "STOP"" MBEYA! Ziara anazozifanya Mchumba wa katibu mkuu wa Chadema JOSEPHINE MASHUMBUSHI mkoani Mbeya zimezua utata baada ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kuzipinga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chadema EDDO MWAMALALA kwa niaba ya wanachama wa chama hicho, alisema ziara anazofanya Mshumbushi mara kwa mara hazina tija katika chama.

Mwamalala alisema mchumba wa Dk. Slaa hana cheo chochote ndani ya chama, hivyo ziara zake haziana baraka yoyote kutoka makao makuuu ya chama na zimelenga maslahi yake binafsi ambayo yanakichafua chama na familia yake binafsi.

""Kimsingi ziara anayofanya Mashumbushi haipo kichama lakini yeye anatumia mwamvuli wa chama kwa kuwadanganya wananchi kusema anatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake huku akiwa ana ajenda binafsi kwa sababu kinachoonekana ni upotoshaji kwa wananchi na chama chetu pia"" alidai Mwamlala.

Alidai kuwa mchumba wa Dk.Slaa si kiongozi wa chama ambaye anastahili kuwa na ziara ya chama kama anavyofanya sasa hata kama ana malengo ya kujenga chama.

Mwamlala alidai kuwa katk ziara hiyo hubeba watoa mafunzo ambao hawana hata kadi za chama lkn hutoa mafunzo kwa wainachama ingawa imethibitika kuwa anakuja nao kwa lengo la kuwanadi huku akiwaahidi kuwateuwa katika ubunge wa viti maalumu.

Alisema ni vema mipango yake akaitofautisha na siasa na harakati za kutetea kundi au jamii fulani na kwamba yeye kama mwanaharakati aachane na uongozi wa chama cha siasa aende kwenye makundi ya asasi zisizo za kiserikali.
HISTORIA YA Mh. Free Man Mbowe.
Mwenyekiti ana historia chafu ya ufuska na uasherati . Hili ni tatizo kwa maadili lakini ni tatizo zaidi kwa Mwenyekiti Mbowe kwasababu analeta hizi tabia kwenye kazi na kuleta mifarakano. Nitatoa mifano kadhaa:

amevunja ndoa ya Mbunge Grace Kiwelu ambaye alikuwa ameolewa na mtoto wa Mzee Ndesamburo anayeitwa Sindato. Mwenyekiti alikuwa na ujasiri wa kulala na Grace...... kwenye ziara za Kichama wakati Mzee Ndesamburo anaona kwa macho yake . Mzee Ndesa alilileta hili suala Kichama, rekodi zipo hadi leo, lakini Mbowe akawa anaendelea. Kesi ilifika mahakamani na talaka kutolewa.

... Mwenyekiti alitia aibu katika ziara tuliyofanya Newala. Grace Kiwelu na Chiku Abwao walipigana usiku saa 7 kwenye nyumba tuliyofikia kwasababu kila mmoja alitaka kulala na Mbowe. Ugomvi ulikuwa mkubwa baadaye Chiku Abwao akafanikiwa kulala na Mbowe. Msafara ulipofika Nachingwea, Grace akawahi kuingia chumbani kwa Mbowe mapema, kwahiyo Chiku akafukuzwa. Ilikuwa ni fedheha kubwa kwa walioshuhudia. Kwa kifupi, kama tunataka kujenga Chama makini, huyu hatufai kama Mwenyekiti. Tunao viongozi wengi ambao hawana historia ya uchafu wa biashara na uchafu binafsi.

Mwenyekiti alipigana na kiongozi mwenzake wa Chama Kawe kwenye sherehe ya kikundi cha sanaa cha Chama kinachoitwa Malongo Sanaa Group kwasababu Mwenyekiti alimtaka msichana mmoja kwenye kikundi anayeitwa Subira Waziri (au Koku) ambaye ni bibi wa kiongozi huyo. Ugomvi huo ulikuwa mkubwa na Mwenyekiti alichaniwa shati, lakini alimpiga na kumuumiza kiongozi mwenzake. Kesho yake Mwenyekiti akaenda kwa Mzee Makani kuomba radhi na kutoa 300,000 kwa kiongozi mwenzake asiseme na kuchukua hatua.

Mwenyekiti pia amevunja ndoa ya Mwanamrisho Abama wa Zanzibar ambaye bado anaendelea naye mpaka leo. Pia ameingilia ndoa ya Sophia Khatau wa Lindi ambaye mume wake anafanya kazi TTCL. Pia alivuruga ndoa ya Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Hai anaitwa Helga
Sorce:
Ufisadi mkubwa ndani ya CHADEMA; ni kuhusu, Ubadhilifu wa Dr.slaa na Josephine, Mamilioni ya Sabodo,
BAADHI YA UBADHILIFU WA DR.SLAA NA MCHUMBA WAKE JOSEPHINE

2. Dkt. Slaa yeye amedhihirisha ni jinsi gani mnafiki kwani pamoja na kujidai kupinga posho lakini bado ameshindwa hata kuusimamia mfumo wa posho ndani ya chama chake nitatoa mfano;-
i. Amelazimisha chama kumlipa mke wake milioni kumi kama malipo ya kutengeneza mfumo wa komputa wa kusimamia mahesabu ya chama.
ii. Anajilipa posho ya shilingi 250000/= kwa siku kila aendepo ziara na kwenye kesi yake kule Arusha ambapo yeye, mke wake pamoja na yaya wao husafirishwa kwa ndege kila safari na wote wanalipwa 250,000/= ya kujikimu wakati wote wanalala chumba kimoja?. Haya ni matumizi mabaya ya ruzuku ya chama ambazo ni kodi za wananchi.
iii. Amejikopesha pesa ya chama kujengea nyumba yake kule kunduchi ambapo yeye mwenyewe ndio msimamizi mkuu wa pesa za chama na ndio mlipaji mkuu na wala hajafuata mfumo wowote wa malipo na ukopeshaji na haijulikani ni lini atarudisha fedha hizo za wanachama na kwa utaratibu upi?.

MAJIBU YA DR.SLAA NI HAYA HAPA
WanaJF,
Slaa hana cha kuficha kwa kuwa utaratibu uko wazi.
1. Kulipwa Mke wa Dr Slaa aweke ushahidi wana Jamvi waupime.
2. Ni kweli Josephine ambaye Professionally ni pamoja na System Analyst ali volunteer ku design Reporting System.
Inawezekana mhusika ameona sasa atabanwa vilivyo hivyo anapiga vita. Nilidhani anayejitolea anapongezwa!.
3. Kabla ya Junior kwenye kesi tulikuwa tukilala Sky Link
au Miami 40،000 per night. Baada ya Junior akiwa miezi 3 Impala at 280،000 per night bila chumba cha yaya na extra za mtoto na chakula. Kesi ni za Chama alitaka tumwadhibu Junior? Inawezekana hajui maana ya kusafiri na mtoto wa miezi 3! Tungekuwa fisadi tungelala Naura Sring, Kibo Palace, Mt. Meru etc. Inawezekana hajui rates za Luxury hotels.
AKAULIZWA TENA
Hapo kwenye red Dr.slaa ni wazi mnapeana mambo n a mchumba wako,cv ya Josephine inaruhusu mambo haya?Hili swala si ndio lile linaloleta mgogoro wewe na anton komu mmiliki wa mwanahalisi(msishangae kuona mwanahali likianza kufichua uovu wa chadema,kwa sababu Anton komu ameamuliwa ajiuzulu,kwa sababu josephine anataka kuchukua nafasi yake pale makao makuu).
NAOMBA DR.SLAA AJIBU TENA HUJUMA HIZI ANAZOZIFANYA NDANI YA CHAMA YEYE PAMOJA NA JOSEPHINE:

1.Hivi unaweza ukatuambia ni kwanini kesi ya chama chako tu ndo igaramiwe na chama wakati kesi ya chama ya susan kiwanga na Kasurumbai wanajigaramia wenyewe?. mbona wewe na hao wote mnalipwa sawa milioni 7 kwwa mwezi?.

2.Unaweza ukatueleza watu wenye akili zetu ulitumia kikao gani kuidhinishiwa mkopo uliojengea nyumba yako ambao unatokana na pesa za wananchama?.

3.Unaweza ukatueleza ni kwanini ulipindisha maamuzi ya kamati kuu ya kuhakikisha kila mwezi chhama kiweke 25% ya ruzuku kwenye akaunti ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi ujao?. unaweza ukasema ni kwanini mpaka hii leo kuna shilkingi 0 kwenye akaunti ya uchaguzi?.

4.Unaweza ukasema ni kwanini wewe ukishirikiana na mapacha wenzako wawili mlikwenda kupindisha maamuzi ya kamati kuu ya kuweka 20% ya ruzuku ya chama kila mwezi kwa ajili ya Investments za chama na mpaka hivi sasa chama hakina hata Baiskeli ya mbao iliyonunua tangu uchaguzi mkuu uishe?.

5.Unaweza ukasema ni kwanini chama kimlipe posho ya 250000 mkeo kila akienda kusikiliza kesi yake pale mahakamani arusha na haimpi hata senti moja Dady Igogo ambaye naye pia ni m,shitakiwa kwenye kesi kama hiyo?.

6.HIVI UNAWEZA KUSEMA MBELE YA WATU KUWA WEWE NI KIONGOZI WA WANYONGE KWELI HALAFU UNALALA HOTEL YA 280000?. Sasa kama ndio hivyo inakuwaje muwalipe wenzenu mliowatuma uzini na arumeru elfu  30 kwa siku au wewe na mbowe ndio mnajua sana kulala kuliko wenzenu?

7.Unaweza ukatuambia ni kwanini House Girl wako alipwe na chama shilingi 250000 kila siku pindi muwapo Arusha wakati hata kadi ya chama hana?.

8.Unaweza ukasema ni kwanini ulimwamuru MWIGAMBA AJIUDHURU baada ya kukataa kulipa milioni 10 za kutengeneza acuonting system za chama?.

9.Unaweza ukasema ni lini tangazo la ma volunteer wanaoweza kutengeneza acoounting system lilitangazwa hapa kwenye ubao wa matangazo wa chadema hadi hawara ako akashinda hiyo nafasi?..
karibu tena utupatie majibu tafadhali....

KUHUSU UBADHILIFU WA MAMILLION YA SABODO

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) ni moja kati ya chama kilichojizolea umaarufu sana hapa nchini na kusema ukweli muundo wa katiba yake na sera zake umekaa kiukombozi haswaa!!!! Wananchi wengi tunaipenda chadema..hasa namna viongozi wake akina Mbowe na Slaa wanavyojua kuhadaa watanzania wanapokuwa kwenye majukwa ya siasa.

Ikumbukwe ni hawa hawa akina Slaa na Mbowe ndio waliotaja List of Shame pale mwembe yanga...walifichua ufisadi mkubwa sana unaofanywa na serikali ya CCM kupitia viongozi wake.

Lakini leo hii inashangaza sana kuona Mbowe na Slaa ndio haohao wanaoongoza kwa ufisadi mkubwa ndani ya chama na kwa watanzania kwa ujumla wao!

WAKATI wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 tunakumbuka wote kuwa Mfanya Biashara maarufu Tanzania SABODO alitoa kwa mara ya kwanza Million 100 kwa CHADEMA ilikuimarisha nguvu ya kampeni na kukijenga chama kipindi chote cha kampeni.

AWAMU ya pili alitoa millioni mia moja (100) kwa ajili ya kujenga chuo pale KIBAHA cha CHADEMA ilivijana wawezekupata mafunzo ya kisiasa, uzalendo ndani ya chama na nchi yao.

Akaahidi kutoa Million 100 zingine kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho pale Kibaha, ambazo kwa mujibu wa ripoti unaonyesha kuwa amezitoa.

AWAMU ya tatu ametoa MIllion Mia Moja (100) kwajili ya ujenzi wa visima miambili (200) katika maeneo ya majimbo yanayoongozwa na wabunge wa chadema.

Jumla ya pesa taslimu aliyoitoa hand to hand ambazo watanzania ni Million mia tatu (300).

LAKINI cha kusikitisha pesa hizo zimeenda kukarabati ukumbi wa starehe unaomilikiwa na MH. Freeman Mbowe ule wa BILLICANAS (Kama unabisha nenda Billcanas ukaone ujenzi unaondelea na fedha zimechotwa kwenye account ya uchaguzi ya chama).

Napia ametumia pesa hizo kwenda kununua nyumba ya kifahari pale DUBAI ambayo hadi dakika hii anaifanyia ukarabati kwaajili ya kuipangisha na kuhamishia baadhi ya ndugu zake pale Dubai.

PESA nyingine toka kwenye account ya UCHAGUZI 2015 imetumika kujengea nyumba ya katibu mkuu Ndugu W.P. Slaa maeneo ya KUNDUCHI (amehamia hapo kunduchi mwaka huu). Kabla ya hapo alikuwa anaishi PALE ABLA APARTMENT Kijitonyama ambapo ameishi kwa muda wa miaka miwili na malipo ya kodi kwa siku ni Tsh.250,000 (laki mbili na nusu, watanzania uzalendo wa Dr.Slaa upo wapi katika hili) ambapo pesa hiyo ilikuwa inalipwa na chama na hapo ndipo matokeo ya mgombea urais yalihesabiwa na kauli ya kwamba tumechakachuliwa ilitolewa hapo.

WAKATI HUO HUO,  Mh. Mbowe amekuwa akiwahadaa watanzania kwa kurudisha gari la kifahari la serikali ambalo ni maalumu kwa ajili ya kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Alirudisha gari hilo kwa mbwembwe kweli na vyombo vya habari vililizungumzia sana jambo hili.

NASASA amelichukua kimyakimya na huku watanzania wasijue kuwa anaendelea kulitumia. Yeye na chama chake walisema hawataki posho za bunge lakini mpaka leo hii mbowe anachukua posho na pia Dr.Slaa anachukua posho akiwa katika kazi za ujenzi wa chama ambayo kwa siku analipwa Laki moja, Dreva wake analipwa 30,000 na mlinzi wake analipwa 30,000 hiyo ni mbali na mshara wa milioni saba (7,000,000) kwa kila mwezi (wakati huo ikumbukwe makati wa kuu wa mikoa wa chama, makatibu wakuu wa wilaya n.k wa chadema hawalipwi chochote, hawapewi posho hata sent moja)...

Na pia kanisa analo sali mchumba wake CHAMA kinawalipa walinzi wawili lakitano kwa mwezi kila mmoja kwaajili ya ulinzi wa kanisa hilo analosali JOSEPHINE MSHUMBUSI.

MAJIBU YA DR.SLAA YALIKUWA HIVI;

Upotoshaji si vema kuuchia. Mnyika yuko Joeburg kikazi hivyo naomba kufafanua mwenyewe.

1. Fedha za Sabodo ni kweli zimepokelewa kwa awamu mbili @ 100m. Hizi zilikuwa kwa ajili ya Kampeni Uchaguzi Mkuu na tumezitolea taarifa ya matumizi mara kadhaa hadharani. Taarifa pia ipo kwa Msajili wa vyama kama mhusika anataka kujua zaidi.

2. Fedha za Sabodo ahadi ya 150m kwa ajili ya ujenzi wa Chuo. Ilikuwa ahadi na hatua tuliyopo sasa ni ku process "title Deed" eneo la ekari 100m Soga, Kibaha. Fedha za Sabodo bado ziko kwa Sabodo kwa kuwa ujenzi haujaanza. Sijui kama Sabodo anaweza kujifisadi mwenyewe.

3. Fedha za visima 200m toka Sabodo. Wajibu wa Chama ilikuwa kuomba. Wajibu wa Sabodo ni survey, design, kuchimba na kukabidhi visima vilivyokamilika ( turn key). Sijui kwenye Turn key project ufisadi una sura gani. Labda mimi sielewi.

4. Nyumba ya Dr Slaa. Hivi mhusika alitaka niishi Abla milele au alitaka nikope kwake ili ajue siyo ufisadi. Anaruhusiwa kupekua pote na aanike hadharani ushahidi wake

4. Sihitaji kumtetea Mbowe. Ni mfanyibiashara asiyejificha. Sources za ujenzi wa Bilicanas si siri aache uvivu wa kufikiri na kutafiti kisayansi.

Nauliza hivi!
1.Uadilifu wa viongozi wa chadema uko wapi?
2.Je huu sio ufisadi? au ufisadi ni EPA, MEREMETA na DOWANS tu?
3.Hivi unapo wadanganya watanzania kuwa umerudisha gari wakati nyuma yake umelichukua kimya kimya inaleta picha gani?
4.Hivi kunautofauti gani kati ya mwamvita makamba aliyejenga nyumba hapa TZ na Mbowe aliyekwenda kununua nyumba nje ya nchi ?
5.Hivi hatari ya kuwaamini viongozi kama hawa ambao machoni niwasafi, moyoni wanaroho ya mbwa mwitu mwisho wake itakuwaje?
6.Hivi kunaulazima gani kuweka walinzi kanisani anakosali mchumba wa Dr.slaa kwa kutumia ruzuku ya chama?
7.Hivi CHADEMA watachukuaje nchi, ikiwa pesa iliyoazimishwa na kamati kuu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kuwa asilimia 25% ya ruzuku yote kwa kila mwezi iwekwe kwenye account ya uchaguzi kwaajili ya 2015, lakini mpaka sasa hakuna hata shillingi zote zimechukuliwa na wajanja wa chache?
8.Josephine mbona anatuharibia chama? Mbona mke wa mbowe yupo kimya?Josephine ni mchumba tu na sio mke rasmi wa Dr.slaa lakini amekuwa na nguvu sana ya kuendesha mambo ndani ya chama?

Source: (Shambani Leo Page @ Facebook)

  • Kusoma comments na kuangalia likes tembelea page ya "Shambani Leo"  Facebook

1 comment:

  1. si dhni kama kuna aliyemsafi katika siasa zetu hizi, kila mtu analilia nafasi kwa kuwa wanaona aliyeikalia hiyo nafasi anakula zaidi nao wanaona wivu

    ReplyDelete

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...