08 June, 2012

Asante Dk. Mwakyembe

Alichokifanya Dk. Mwakyembe ni kitu cha kuigwa na mawaziri wengine katika wizara zao kwani kuna mambo ya hovyo sana, yaani CEO anaidhinisha dola 50,000 kwa ajili yakutengeneza uniform pair 17 nchini China??!! Tena na kuwapeleka maafisa 2 kwaajili ya kusimamia ushonaji??!! Huu ni wizi mkubwa hawa watu washtakiwe kabisa, pia Waziri usiishie hapo tu nenda na kule mamlaka ya Bandari kuna madudu kweli huko, mwisho hakikisha usafiri wa reli unafunguka sehemu zote hii itasaidia sana kupunguza gharama za usafirishaji, chapa kazi bila kuogopa mtu DK.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...