04 August, 2012

JB NA AUNT EZEKIEL WAPATA ULAJI,,!


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Wasanii mashuhuri wa sanaa ya filamu hapa nchini Jacob Steven 'JB' na mwanadada anayeng'aa Aunt Ezekiel wamepata ulaji na kampuni ya ZUKU ambayo inahusika na maswala ya ving'amuzi vya Tv zikiwemo channel ambazo zinaonesha filamu za Kitanzania kwa sasa. Wasanii hao wamechaguliwa na kampuni hiyo kuwa mabalozi wao kwa upande wa tasnia ya filamu na nchi ya Tanzania kwa ujumla ambao sasa filamu zao zitakuwa zikioneshwa kwenye king'amuzi cha kampuni hiyo huku nyingi zikiwa kutoka kwa wasambazaji mahiri hapa Tanzania wanaojulikana kama
Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam ambapo lengo jingine la kufanya hivyo ni kuikuza lugha ya Kiswahili kupitia filamu zetu hapa nchini ambazo zitakuwa zikionekana dunia nzima kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...