Majira ya mchana leo msanii wa muziki wa kizazi kipya Roma Mkatoliki amepata ajali ya gari baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Morogoro kupata pancha na kuhama njia yake hali iliyosababisha gari hilo kugongana na gari jingine aina ya Fuso. Msanii huyo alikuwa akiendesha gari lake kwenye mwendo wa kawaida lakini ghafla tairi ya gari lake ilipata pancha na kupelekea ajali hiyo, Msanii huyo alikuwa anaenda kwenye show yake mjini huko akiwa na rafiki zake na hakuna yeyote aliyeumia wala kufariki kwenye ajali hiyo.
Hapa akitoa maelezo kwa polisi,
Gari hiyo baada ya ajali,
Baadhi ya rafiki wa Roma waliokuwa kwenye gari hiyo,
CHANZO; Djchoka
No comments:
Post a Comment