16 July, 2013

Samora Julius afunguka SHONZA, MWAMPAMBA, MWIGULU SI SULUHISHO LA KERO ZA WANA-ARUSHA.

Wana Ccm sasa wamehakikisha, wametambua, wameelewa kuwa siasa za kanda ya kaskazini ni siasa nyingine si linganifu na siasa za pahala pengine. Ushindi wa viti vinne vya udiwani kwa Chadema si USHINDI mkubwa kwao kwani walijua UCHAGUZI ule ulikuwa mechi ya nyumbani, na kurudia UCHAGUZI ule ulitokana na maamuzi yao ya kuwafukuza madiwani wa chadema kwa kukaidi maagizo HALALI ya kamati kuu ya chadema. Na walifikia maamuzi hayo magumu wakijua kabisa hata uchaguzi ungerudiwa siku yeyote wangeshinda tu! Swali la kujiuliza ni kwanini chadema wanajeuri ya kisiasa Arusha? Majibu yanaweza kuwa mengi kila mtu na lake lakini jibu la msingi ni kuwa wana Arusha wanauelewa mpana, wameelimishwa na wakaelimika, wmefundishika kuwa serikali tulivu ya CCM iliyokaa madarakani kwa miaka 50 ndiyo chanzo kikubwa cha UMASKINI wao. Wao kukosa Huduma ya afya bora, elimu bora, miundombinu ya barabara bora, kupanda kwa gharama za maisha zinatokana serikali ya Ccm. Na wakaelezwa kuwa fedha zao zinazoibwa kupitia miradi mbalimbali Kama EPA, DEEP GREEN, KAGODA, DOWANS, MEREMETA n.k zinatumiwa na viongozi wa serikali ya Ccm na familia zao huku wakiacha maelfu ya Watanzania wakifa kwa kwashakoo, utapyamlo, wakifa kwenye foleni ya matibabu kwa kukosa elfu mbili ya kununua dawa ya kuharisha! Huku viongozi wao wakipigana vikumbo uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere wakielekea hospitali yao ya rufaa Apollo nchini India kutibiwa malaria huku wakiambatana na mashosti, ndugu jamaa na marafiki. Wana Arusha wanajua kuwa mashangingi ya viongozi wao yanauzwa milioni 80 lakini viongozi wa Ccm wameengeza mpaka yamefikia milioni Mia tatu, Pesa ya mlipa kodi! Wameelezwa na viongozi wengine( HOSSEA) kuwa serikali haitaki kuwafikisha mahakamani viongozi wala Rushwa, Mafisadi. Wanajua Tz ndio nchi pekee ambayo mwizi anapewa mda wa kutafakari, kujitathimini ili arudishe fedha alizoiba!
Cha kushangaza Ccm wanamtuma MWIGULU NCHEMBA, SHONZA, MWAMPAMBA, kwenda kuwaeleza wakazi wa Arusha kuwa chanzo cha matatizo yao, umaskini wao ni kwa sababu ya MAANDAMANO, LEMA na CHADEMA!!. Wakasahau kuwa wapiga kura wa Arusha wanaojitambua, wanajiielwa na kuwa adui wao namba moja ni CCM na serikali yake! Mbaya zaidi vikafanyika vikao vya hadharani na faragha vya kueneza uwongo kuwa Arusha haitaendelea kwani chadema wapo nyuma ya mabomu, mauaji, ukatili, umwagaji wa Tindikali. Wakaendelea kuwachonganisha na Wamasai mpaka ikafika hatua kikao cha ma-LAIGWANANI kikaitishwa chini ya ufadhili wa Ccm wakatangaza kuwa watawafukuza WACHAGGA Arusha kwa sababu wanaleta fujo, maandamano pasipo kujua mbinu ile ilikuwa chafu kwani hata WACHAGGA ambao ni Ccm hawakupigia CCM kura kwa hasira. Wana Arusha wanajua kuwa CHADEMA ni Chama kilichowakomboa kifikra, ni chama pekee kinachoifanya serikali kuwajibika kwa wananchi, ni chama kinachotetea maslahi mapana ya taifa, ni chama kinachojitanabaisha na wananchi. Ccm hata waende taifa gani kumpata mshauri mwenye shahada za uzamivu Mia Tisa, vyeti vya propaganda tani nne. Kamwe hawataweza kuwashawishi wana Arusha kuwa CHADEMA ni chama hatari, Chama cha matukio, chama cha maandamano, chama cha kidini, chama cha WACHAGGA na kadhalika. Ccm wao waharakishe maendeleo kwa wana Arusha wajenge miundombinu bora, watoe huduma ya afya bora, elimu bora hakuna mtu atatafuta mbadala wa CCM. SHONZA, MWAMPAMBA, MWIGULU hawawezi kubadilisha watu wanaojitambua kwa Kutoa matusi, kejeli na kutoa kauli tata kuwa msipoichagua Ccm watakiona cha MOTO,

NICHUNGU LAKINI DAWA

(Kidumu Chama tawala CCM)

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...