05 August, 2013

AZAM TV NA KIZAA ZAA CHA YANGA

AZAM TV; nimekuwa nikifuatilia sana wanotetea hoja za YANGA dhidi ya AZAM TV, nimekuwa msikivu sana lakini kuna maeneo naona mnatawaliwa nahofu tu sio kingine. kwa mfano suala la Azam Tv na Azam Fc, hebu angalieni Supersport Tv na Supersport United. Pili, Yanga inanung'unika kurushwa mechi hizo LIVE kutapunguza mapato sababu inategemea viingilio hivyo vitapungua (mungu wanguuu!). tatu, tunapolinganisha na nchi za Ulaya ktk maendeleo ya soka, tujipime na uendeshaji wetu. nne, suala la mgongano wa maslahi kwa Wallace Karia Mkuu wa Kamati ya Ligi na Said Mohamed Mkurugenzi wa Makampuni ya Azam, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi. najiuliza shida iko wapi kwa hawa kwenye suala hili? hofu ya nini? je waliingiaje kuongoza kamati ya ligi kuu? hebu tumtazame David Gill ataipendelea Man united pale FA au atafuata sheria? je Karia na Said Mohamed hawkuchaguliwa kisheria?
@wazo tu hili, sina upande wowote ila nazingatia kanuni zilizotumika, ruksa kunielimisha,

By Markus Mpangala

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...