27 September, 2013

AJALI MBAYA KATI YA LAND CRUISER NA PIKIPIKI...TAHADHARI: PICHA ZINATISHA


Ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo majira ya saa 2 kwenye barabara ya majita karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini Musoma kuelekea kamnyonge.





Kamera yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali. 





Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia abiria alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.


Chanzo: shebbyd
 


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...