Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete Siku ya Ijumaa, Septemba 20, 2013, alitunukiwa Shahada ya
Uzamivu (PHD) na Chuo Kikuu cha Guelph cha Canada kwa kutambua mchango na
uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa
Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso.
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe
baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni
Ontario jana

No comments:
Post a Comment