18 September, 2013

KITENDO CHA H-BABA KUVUJISHA PICHA ZA MKEWE AKIJIFUNGUA CHAWAKERA WATU.


Flora Mvungi (Hadija) akijifungua. Kutoka kwa vyanzo vyake, mbali na picha za mtoto, Mwandishi wetu alilibamba tukio la Flora akijifungua
Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Marie Stopes iliyopo Sinza, Dar.



.
 Flora akiwa hospitali na mumewe H. Baba. Kwa mujibu wa H. Baba, alifurahishwa kuitwa baba kwani ni kitu ambacho alikuwa anatamani kwa muda mrefu na Mungu amemtimizia hivyo anamshukuru kwani ni zawadi kubwa katika maisha yake.

 Mtoto wa Flora Mvungi.
Kwa upande wa Flora alikuwa na haya ya kusema: “Namshukuru sana Mungu kwa sababu niko salama na mwanangu, ukweli mwacheni mama aitwe mama kwani kuzaa siyo kazi rahisi”.

H. Baba alimalizia kwa kusema kuwa kama walivyosema awali kabla mtoto huyo hajazaliwa kuwa jina lake ataitwa Tanzanite, ndiyo hivyo itakavyokuwa jina hilo ndilo litakalotumika.
Lakini katika hali nyingine watu mbalimbali wamemponda H Baba kwa kuzivujisha makusudi picha za kitoto hicho kichanga" Huyu H Baba hajielewi kabisa kwa nini anamdhalilisha mwanae hata siku 2 hajamaliza kesha aanza kumning'iniza kwenye vyombo vya habari huu ni ushamba na upuuzi" Alisema Mama Hemed wa Kinondoni Stereo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...