31 October, 2013

DIAMOND: 'NILIFUNGWA SABABU YA KUGOMBEA DEMU, HIVYO SIOGOPI KURUDIANA NA WEMA NA SITISHIKI'



                                      Nasibu Abdul ‘Diamond’


STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewahi kusota lupango ya Keko, Temeke jijini Dar es Salaam kwa miezi miwili kisa kikiwa ni kugombea demu wa mtu.
Diamond alisema tukio hilo lilimtokea mwaka 2007 akiwa ‘andagraundi’ wa muziki wa kizazi kipya.
Diamond aliyasema hayo kufuatia kuulizwa swali kwamba, amerudiana na Miss Tanzania 2006 ambaye pia ni staa wa filamu za Bongo, Wema Sepetu. Je, haogopi kufanyiwa kitu mbaya na jamaa wake ambaye ndiye anayemuweka mjini?
Msikie Diamond: Mimi simwogopi mtu eti kwa sababu natembea na demu wake. Hakuna anayeweza kunifanya lolote lile, najiamini.
“Mwaka elfu mbili na saba niligombea demu na jamaa mmoja pale Tandale (Dar). Matokeo yake jamaa akanikamata na kuniweka Gereza la Keko kwa miezi miwili, nikaachiwa baadaye, kwa hiyo sitishiki,” alisema Diamond.
Hata hivyo, Diamond hakuweka wazi kwamba baada ya kukamatwa alipelekwa kituo gani cha polisi na mahakama gani alipandishwa kabla ya kupelekwa mahabusu ya Keko.

Na Shakoor Jongo

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...