04 November, 2013

SHIBUDA AFUKUZWA KWENYE KIKAO CHA CHADEMA BAADA KUDAIWA KUWA KIBARAKA WA CCM

Kikao kinachojadili maendeleo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya ziwa Mashariki (Mara,Simiyu na Shinyanga) kimemtimua Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye muda mfupi uliopita jioni hii.

Shibuda ambaye alihudhuria kikao hichou kama mbunge wa Kanda hiyo alijikuta akipatwa na zahama hiyo baada ya mjumbe mmoja kutoa hoja kwa Mwenyekiti wa Kikao hicho kwamba Shibuda atoke nje.

Mjumbe huyo alisema Shibuda ni mamluki na kibaraka wa CCM hasa kutokana na matamshi yake kadhaa dhidi ya Chadema na mwenendo wake usioridhisha ndani ya chama.Aliongeza kwamba Shibuda alikuwa kwenye kikao hicho kwa lengo maalum la kukusanya habari na kupeleka CCM.

Hatimaye hoja ya mjumbe huyo iliungwa mkono na wajumbe wote na hatimaye ikapigwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Shibuda alikubali kuondoka ndani ya kikao hicho kwa aibu kubwa na hatimaye mkutano umeendelea!

Source:JF

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...