“Tumepata
barua kutoka kwa kampuni ya Pan African inayotuuzia gesi, wakisema inafanya
matengenezo hayo kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa
yakikosa umeme,” alisema.
Kwa
mujibu wa Masoud, kutokana na matengenezo hayo mikoa iliyounganishwa katika
gridi ya Taifa itaathirika kwa kukosa umeme kwa baadhi ya maeneo na kwa nyakati
tofauti na kuongeza huduma ya umeme ni muhimu kwa kila Mtanzania kwa ajili ya
kujiinua kiuchumi na kipato, lakini matengenezo hayo ni muhimu kwani itaboresha
upatikanaji wa gesi kwa ufanisi zaidi.
Aliitaja
mikoa na maeneo yatakayokumbwa na upungufu wa umeme kuwa ni Dar es Salaam,
Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Morogoro, Singida, Mwanza, Mara,
Mbeya, Iringa, Tabora, Shinyanga, Manyara na Zanzibar.
Masoud
alisema gesi imekuwa ikiwawezesha kutoa Megawati 100 katika kituo cha Ubungo 1,
Megawati 100 katika kituo cha Ubungo 2, kituo cha Tegeta Megawati 45 wakati
Kampuni ya Songas imekuwa ikitoa Megawati 182 na kuongeza kutokana na
matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa Megawati kati ya 150 na 200 na kwamba
uzalishaji wa umeme kutumia mafuta na maji utaendelea.
Alisisitiza
kuwa upungufu huo wa umeme sio mgawo ila ni kupitisha matengenezo ya kiufundi
ya Kampuni ya Pan African ambayo alidai kuwa ilishaiomba Tanesco miezi miwili
iliyopita ikitaka kufanya matengenezo hayo ambayo hayaepukiki na yenye lengo la
kuleta ufanisi zaidi.
Masoud
alitoa wito kwa wananchi kuwa wavumilivu siku hizo 11 wakati matengenezo
yakifanyika na kuwa lengo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwa ajili
ya kuzalisha umeme wa kutosha na kutoa huduma inayoridhisha ya nishati ya umeme
kwa wateja wake.
-Habari Leo
-Habari Leo
No comments:
Post a Comment