Baadhi ya Wataalamu wa kufichua watu wanaojihusisha na
vitendo vya ushirikina na uchawi maarufu KAMCHAPE wamejikuta wakiwa kwenye
mikono ya dola baada ya kuendesha zoezi la kufichua uchawi katika nyumba kadhaa
kwenye vijiji mbalimbali vya manispaa ya Tabora ambapo baadhi ya wananchi
walililalamikia zoezi hilo kwa madai kwamba limekuwa likiwadhalilisha baadhi ya
watu pamoja na kujenga chuki ambazo huenda zikasababisha madhara makubwa katika
jamii.
Hapa ni baada ya kufikishwa kituo kikubwa cha Polisi
mjini Tabora kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya ambapo
aliwataka kuacha mara moja zoezi hilo la kufichua wachawi
No comments:
Post a Comment