15 January, 2014

‘B 12’, ‘DIVA’ & ADAM MCHOMVU OUT CLOUDS



WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamisi Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na  Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na kituo hicho!



Habari za chini kwa chini zinasema kuwa, uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu kwa watangazaji hao.


Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba, watangazaji hao wamesimamishwa kwa kosa la kukacha sherehe za  maadhimisho ya Miaka 14 ya Clouds FM,  yaliyofanyikia hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.



Chanzo cha habari hii kilimvutia waya, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Muhatahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.

“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.

“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana, ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.

Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usijulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.”

Credit Musa Mateja 

       


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...