Mwanzoni wakati
nnafungua blog ya JoJoTheFighter; nakumbuka vizuri sana ilikua ni assignment tuliyopewa na lecturer
Agness Shija (kwa sasa ni marehemu )
kupitia course aliyokua akitufundisha ya
International Mass Communication,
katika chuo kishiriki cha Tumaini kilichopo Dar,
wakati huo ndio tulikua tumehamishiwa Mikocheni kwa Warioba baada ya kuhama kutoka Kinondoni. Kwa
sasa nasikia kimehamishwa tena , na sasa kipo Mwenge!
Kiukweli kwa
wakati ule mimi na wana chuo wenzangu (sio wote) tuliona kama usumbufu… si
unajua tena mambo ya assignment yalivyo
na stress hasa linapokuja swala la deadline? Assignment aliyokua ametupa Madam Shija ilikua ni kufungua blog na
ku post habari kisha tumtumie link ya blog kwenye email address yake
ili aweze kutoa marks!
Jumapili ya Tarehe 11 August 2013 asubuhi, nilipatwa na pigo kubwa baada ya kusikia
taarifa ya kifo chako! Huko ulipo kama unanisikia, nakupa shukrani toka moyoni. Nakumbuka ucheshi wako, ushauri na juhudi zako zilizonifanya nijifunze mengi kutoka kwako.
Ni miaka mitatu
sasa imepita tokea assignment uliyotupa
igeuke matunda na kunifanya nipate kipato bila kutumia nguvu kupitia blog! Asante sana Madam.
No comments:
Post a Comment