WILAYA YAMOMBA –MAUAJI
MNAMO
TAREHE 11.01.2014 MAJIRA YA SAA 03:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
SAMANG’OMBE, KATA YA IVUNA, TARAFA
YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA, MSAFIRI S/O DAIMON,
MIAKA 22, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA RWATWE ALIUAWA KWA KUCHOMWA
KISU TUMBONI NA UTUMBO MKUBWA KUTOKA NJE NA
BOIDI S/O PASCHAL, MIAKA 36, MNYAMWANGA ,MKULIMA NA MKAZI WA
RWATWE.CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI/UGONI
BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MKEWE KILABUNI.MTUHUMIWA
AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI INA MADHARA MAKUBWA
NA BADALA YAKE WATUMIE NJIA ZA BUSARA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YAO INAYOWAKABILI.
WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA
NA BHANGI
MNAMO TAREHE 11.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:30HRS
HUKO KIJIJI CHA KAPELA, KATA YA MAKWALE, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA,
MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA/MSAKO WALIMKAMATA LIVING S/O JEKE,
MIAKA 27, MKULIMA NA MKAZI WA KATALE AKIWA NA BHANGI KETE 14 NA GRAMU 250,
BHANGI YOTE IKIWA NA UZITO WA GRAMU 320.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA
MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA PIA NI HATARI KIAFYA KWA WATUMIAJI.
Credit:
No comments:
Post a Comment