RAIA
watatu wa Nigeria na mwanamke wa Kitanzania wamekamatwa na polisi jijini Dar es
Salaam, wakituhumiwa kujaribu kusafirisha madawa ya kulevya kwenda nchini
Liberia. Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa mbioni kutuma mihadarahi hiyo,
ikiwa kwenye vitabu, kwa kutumia Wakala wa Usafirishaji Mizigo ya DHL.Kamanda
wa Polisi, Kanda Maalumu Dar es Salam, Suleiman Kova alitaja majina ya
Wanaijeria hao kuwa ni Sunday Chaidikaobi (42), Chukwuma Favour (31), na
Franklin Indubuisi (41). Mtanzania aliyebambwa pamoja na Wanaijeria hao
ametajwa kuwa ni bi Hadija Ngoma (43), mkazi wa Kimara Temboni, Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kova, polisi walipata taarifa juzi, Machi 18, kuwa kuna watu
wanne wanajihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya waliokuwa katika ofisi
za DHL zilizopo Barabara ya Sam Nujoma.
Kufuatia
taarifa hizo, Kamanda Kova amesema “makachero walifuatilia suala hilo na
hatimaye siku hiyo saa 8:30 mchana watu hao walikamatwa wakiwa na kifurushi
wakijiandaa kukisafirisha kwenda nchini Liberia.”
Alisema
polisi walipopekua kifurushi hicho, walikuta vitabu vitatu vya Kiingereza.
Walipopekua vitabu hivyo, walikuta madawa aina ya heroin katika kurasa za
mwanzo.
“Katika
vile vitabu kurasa ya kwanza inayofunika lile jalada gumu kwa ndani, walikuwa
wamefunua na kuweka unga huo na katika ukurasa wa nyuma vivyo hivyo kwa vitabu
vyote,” aliongeza.
Unga
huo unaokadiriwa kuwa na uzito wa nusu kilo, umepelekwa kwa mkemia mkuu wa
serikali kwa uchunguzi zaidi kubaini thamani na uthibitisho wa madawa hayo.
Inaonekana
Wanigeria wanakuja kwa kasi kwenye biashara hii ndani ya Afrika Mashariki.
Miezi kadhaa iliyopita, Wanigeria wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya, wakijaribu kusafirisha dawa za kulevya
aina ya cocaine zenye thamani ya takriban shilingi milioni 120; kama
inavyoonesha video hii hapa chini
No comments:
Post a Comment