Katibu Mwenezi wa CHADEMA Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki amejiuzulu
![]() |
Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia Jiji la Mbeya Lucas MwampikiKatibu
Mwenezi wa Chama cha Demokrasia Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki amejiuzulu
wadhifa huo kuanzia Aprili mwaka huu kutokana na mkanganyiko wa uongozi
ndani ya chama hicho.
Mwapiki
amesema amechoshwa na malumbano ya mara kwa mara na meza kuu ndani ya
chama hicho katika ngazi ya wilaya hivyo kudhoofisha juhudi zake za
kukijenga chama hicho.
Aidha
Mwampiki amesema viongozi wa chama hicho wamekuwa na malumbano ya mara
kwa mara hivyo yeye kama kiongozi hayupo tayari kuona mambo yanavurugika
katika chama hicho.
Hata
hivyo katika uamuzi aliouchukua Lucas Mwapiki amesema kuwa yeye
atabakia kuwa mwanachama wa chama hicho na Diwani wa Kata ya Mwakibete
Jijini Mbeya.
Amewataka
wanachama wamuelewe hivyo ameona yeye akae pembeni badala ya kuwa na
muda mwingi wa kujadili migogoro ambayo haina tija na kuleta mkanganyiko
kwa wanachama.
|
No comments:
Post a Comment