27 April, 2014

HAFLA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA VIWANJA VYA IKULU

1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakikata keki katika sherehe ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili 26 mwaka 1964 hafla hiyo iilifanyika jana kwenye viwanja vya Ikulu na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Seif Ali Idd, Waziri Mkuu Tanzania Mh. Mizengo Pinda na viongozi mbalimbali wa serikali taasisi za dini na vyma vya siasa, Kushoto ni Mke wa Rais mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkewa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein3Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakiwalisha keki wake zao katika hafla hiyo. 4Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kifaa maalum cha kufyatua mafataki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

23 15gRais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein kulia, Dr. Gharib Bilal Makamu wa Rais wa pili kutoka kulia ni Balozi Seif Ali Idd Makamu wa pili wa Rais Zanzibar wakiongoza watanzania katika hafla hiyo. 16Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti Kijana Calvin Nyoni Mshindi wa Musiki wa kizazi kipya kwa ajili ya sherehe za Muungano wa Tanzania 18Kikundi cha muziki kikiburudisha katika hafla hiyo kwenye viwanja vya Ikulu. 19Babu Tale Meneja wa Diamond kushoto nia Mkubwa Fella kiongozi wa kundi la TMK Family walikuwepo pia. 20Kulia ni Mzee Nyantori kutoka Idara ya Habari Maelezo Mdau Cliford Tandali katikati na Nyakia kutoka CCM Makao makuu. Waziri wa Habari, Maendeleo ya Vijana Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara akizungumza na Mhariri Mtendaji wa TSN Bw, Gabriel Nderumaki na mdau Mabhare Matinyi katikati.  24Wake wa viongozi 26Rais wa Jamhuri ya Muungano pamoja na wake wa viongozi wakifuatilia burudani 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...