29 April, 2014

HASSAN MBANGWA KUFUNGUA CHUO CHA UTENGENEZAJI WA VIDEO ZA KISASA MWAKANI!!

 
Hassan Mbangwa
Mkali wa upigaji picha wa video za muziki na filam nchini Tanzania Hassan Mbangwa, anatarajia kufungua chuo kitakachotoa mafunzo ya upigaji picha wa kisasa na kwa kiwango cha kimataifa mapema mwakani. Hivi sasa yupo katika ufuatiliaji wa kufanya usajili wa chuo hicho.

Aidha, jioni hii nimeweza kuzungumza nae kwa kirefu kwa njia ya simu na kuniweka wazi juu ya dhamira yake hiyo njema kwani anaamini kuna mambo makubwa zaidi anaweza kufanya kupitia tasnia hii ya burudani za filamu na video za muziki. 

Hassan Mbangwa kupitia kampuni yake ya Brayance Works, amefanya vizuri sana katika video za wasanii wakubwa wa Injili wakiwemo Rose Mhando, Bahati Bukuku na wengine kibao huku akiendelea kujizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania.



Hizi ni baadhi ya Video alizofanya Hassan Mbangwa....




Blog ya JoJoTheFighter inamtakia Hassan Mbangwa kila la heri katika harakati zake za kufungua chuo hicho kitakachowasaidia watu wengi kupata ajira na kujiajiri. Blog hii ina ahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali katika kutimiza malengo yake.... KILA LA HERI BROTHER!!!....JoJo Pamoja nawe katika harakati hizo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...