Mchungaji Joseph akiwa stendi ya Ubungo
Kuna
mtumishi kutoka Kenya yuko Dar es salaam anajulikana kama Mchungaji
Joseph, amekuwa akizunguka vituo mbalimbali vya daladala akihubiri
habari za Mungu na kusema mambo mbalimbali anayoyaita ni siri za shetani
na kazi anazozifanya! Pia ni kwa jinsi gani watu wanachukuliwa
misukule!
Mtumishi huyu alielezea aina ya nguo ambazo zimetengenezwa
kuzimu na Mtu akivaa hizi zenye wanyama hawa, huonekana moja kwa moja
kwenye ramani ya kuzimu
Alielezea kwamba aina ya nguo hizi mtu akivaa haishi miaka mingi, au kufa kifo kisicho cha kawaida
Pia alielezea huyo mnyama yupo anaishi baharini hivyo hiyo siyo picha tu!
Pia
kulikua kuna kitambaa ambacho kilikua na alama mbalimbali ambazo
anasema wanatumia wanaoabudu shetani au Freemasons. Na kusema pia wapo
watu wanaosema ni wakristo wanatumia baadhi ya hizi alama hizi kwa kujua
au kutokujua!
Pia
lisema kuna wahubiri wawili ambao wanahubiri kwenye TV wanahubiri na
kuponya kwa nguvu za giza ambapo wanatumia PETE zenye nguvu za giza .
Ameliasa kanisa kuombea kazi ya Mungu kwa kumaanisha maana wapo watu
wamejiingiza kanisani kama kondoo kumbe ni mbwa mwitu.
Alipokua
akihitimisha mahubiri yake, alitaka watu watoe mafungu yao ya kumi na
sadaka, pia aliwaombea wote waliokua na mahitaji mbalimbali.
No comments:
Post a Comment