Msemaji
wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam Tanzania, Rajab Katimba kushoto
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam na kutoa tamko na
kumtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, William Lukuvi kuomba radhi
Waislam kutokana na kauli aliyoitoa Kanisani wakati wa Bunge la Katiba
likiendelea dhidi ya Waislam.
April
17 2014 Wajumbe walio upande wa (UKAWA) kwenye bunge la katiba
wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba waligoma na kuamua kutoka nje ya
bunge hili hapa Dodoma baada ya Profesa Lipumba kumaliza kuzungumza
kwamba hawawezi kuendelea na bunge la matusi na ubaguzi.
Kingine
kikubwa alichozungumza Prof. Lipumba ni kusikitishwa na kauli ya Waziri
Lukuvi aliyoitoa kanisani weekend iliyopita kwamba jeshi litatawala
nchi ambapo April 14 2014 gazeti la Mwananchi lilimnukuu Waziri Lukuvi
akisema Kanisani ‘tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi’
‘Ni
kweli kwamba kikao hichi nilipanga nisichangie kwa sababu niliona mechi
kali tukishindilia watu watakufa, sikusikia vizuri yaliyotokea jana ila
mimi sio mnafiki, nampongeza sana Mh. Mrema kwa hotuba yake juzi, Mrema
ndio mpinzani wa kweli, alisema angalia mambo yanayotokea Znz msidhani
yataishia Magogoni’
‘Baada
ya hotuba ya Rais, mh. Seif Sharrif Hamad alihutubia, yeye ni mchochezi
wa hovyo kwa kumsingizia Rais, hakuna mtu yeyote anaweza kunizuia
kusema ninayoyaamini mimi, sio hapa wala mtaani, ni kweli Jumamosi
nilimwakilisha Waziri mkuu ambae hakunipa hotuba na mambo yalinoga
nikatawazwa kuwa chifu’
‘Viongozi
wa dini waliliombea Bunge pale Kanisani, mimi Waziri nipo pale…
nisiongee chochote??!! tukiendeleza ambayo hayako kwenye mila zetu Znz
na Tanganyika inaweza kuwa kama Korea kaskazini na kusini, hofu
niliyonayo ni juu ya rasimu yenyewe kwa sababu kwanza imejengwa kwenye
misingi ambayo siiamini’
‘Zanzibar
inatambulika kama nchi kwenye katiba yao toka hata kwenye katiba ya
nyuma kabisa, yapo mapungufu muundo wa serikali 3, ukisoma rasimu
wanasema serikali ya Tanganyika imevaa koti la muungano lakini koti
lenyewe tunapokezana, leo anavaa Mwinyi, leo anavaa huyu’
‘Hatujawahi
kutoa bajeti inayotosha kwa jeshi la Wananchi, mmeshawahi ona
wanaandamana kudai haki zao? nina miaka zaidi ya 50 na nisingependa
kuiona Tanzania hii inakwenda kwenye maisha ambayo sikuyazoea ili
kuepusha haya tusijaribu tusichokijua, hii ni hofu yangu… hakuna wa
kunizuia kutoa hofu yangu’
‘Ukweli
ni kwamba kama umesoma hii rasimu, muundo unaweza kuwa umeandikwa
vizuri lakini hauwezi kuwepo, Rais hakutoa vitisho bali mawazo yake kama
Mtanzania, hawa jamaa wamekubaliana, serikali ya Znz wachukue CUF, bara
CHADEMA na muungano waachiwe CCM’
No comments:
Post a Comment