23 April, 2014

KOMBA: ZIKIPITA TATU NAINGIA MSITUNI


Captain John Komba akichangia Bungeni amedai Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili. Wabunge wa CCM ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wanasheria, Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawajatoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba
Sasa, kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote.
-Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim,Mzee Butiku na Mzee Warioba bado ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere.
-Huwezi kusema unamuenzi Mwalimu Nyerere kisha ukakubaliana na kauli za kifedhuli na vitisho vya kipuuzi kabisa vya Captain Komba .Bila aibu wabunge na mawaziri wanashangilia?
-Sasa natoa Rai kwa Viongozi na wafuasi wote wa UKAWA,tusikubaliane hata kidogo na Amri zinazotolewa na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano yetu.Kumbe kuzuia mikutano na Maandamano ni katika kutimiza malengo yao na kuminya haki za kiraia na kidemokrasia?
Katika mchakato huu wa kudai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili tulitakiwa kujadiliana kwa hoja na sio vitisho.
Captain Komba na CCM wenzake pamoja na Mawaziri waliokuwepo Bungeni leo watambue kuwa ndani ya Jeshi la Polisi kuna Askari wanaoguswa na harakati za kudai Tanganyika huru na Zanzibar Huru.
Ndani ya Jeshi la Wananchi watambue kuwa kuna Wanajeshi tena vijana wanaoguswa na hoja za kuidai Tanganyika huru na Zanzibar huru
-Nje ya jeahi na nje ya Bunge lipo jeshi kubwa la wananchi na hasa vijana wanaojiandaa kuidai Tanganyika Huru na Zanzibar huru
-Zama za kulazimisha Muungano wa serikali mbili kwa Vitisho zimekwishwa
-Captain Komba,wabunge na Mawaziri waliopo Bungeni leo wametuonyesha njia kwa rangi zao halisi.Tusirudi nyuma na tusiogope
Msimamo wangu huu utaendelea kubaki hivyo hadi pale Captain Komba atakapofuta kauli yake au atakapochukuliwa hatua kali kwa kauli hizi.
Aluta continua,Victory Ascerta....!
Tusiogope ku-share(Sambaza).

By: Ben Wa Saanane

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...