IDADI ya
vifo vilivyotokea kufuatia ajali mbaya ya basi la LuhuyeExpress
linalofanya safari zake kati ya mji wa Tarime mkoani Mara na Jijini
Mwanza iliyotokea April 21 mwaka huu majira ya saa 5:11 asubuhi katika
kijiji cha Itwimila wilayani Busega mkoa wa Simiyu imeongezekana kufikia
15!
Taarifa
iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, KamishinaMwandamizi wa
Polisi(SACP), Charles Mkumbo kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa idadi
hiyo imeongezeka kufuatia kufariki kwa majeruhi wanne wa ajali hiyo
waliokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali yaRufaa ya Bugando.
Kamanda Mkumbo aliwataja marehemu ambao hadi sasa wametambuliwa kuwa ni Mohama Kidela (32) mkazi wa Bugarika Jijini Mwanza, AlexMasatu(42) mkazi wa Musoma,Wangwe Morice (30) Afisa Elimu Msaidizi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mahemba Chacha (42) mkazi waSerengeti mkoani Mara, Thomas Mwita(40) ambaye ni Mchungaji wa kanisa la SDA mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Wengine ni Esther Morice (18) mkazi wa Tarime mkoani Mara, Rose Willison (21)
mkazi wa Igoma Jijini Mwanza, Shepa Msongoma (58) mkazi wa Nassa Wilayani
Busega na Mtoto Baarka Alex (1) ambaye makazi yake hayajajulikana.Kamanda Mkumbo aliwataja marehemu ambao hadi sasa wametambuliwa kuwa ni Mohama Kidela (32) mkazi wa Bugarika Jijini Mwanza, AlexMasatu(42) mkazi wa Musoma,Wangwe Morice (30) Afisa Elimu Msaidizi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mahemba Chacha (42) mkazi waSerengeti mkoani Mara, Thomas Mwita(40) ambaye ni Mchungaji wa kanisa la SDA mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Pia Kamanda Mkumbo amewaomba watu mbalimbali kufika katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza ili kuweza kutambua miili ya ndugu zao kwani hadi sasa maiti sita bado hazijatambuliwa.
Majeruhi 33 bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza na majeruhi 11 bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani humu linamshikilia mmiliki wa basi hilo, Masalu Jackson mkazi wa Majengo mjini Bunda mkoani Mara ambaye alikamatwa wilayani Busega mkoani humu kufuatia ushirikiano wa jeshi la polisi na wananchi huku wakiendelea kumtafutaaliyekuwa dereva wa basi hilo ambaye jina lake halijapatikana kwasababu alitoroka mara baada ya ajali kutokea.
Basi la Luhuye Express lenye namba za usajili T 410 AWQ liliacha njia na kugonga nyumba ya marehemu Mwalimu, Lazaro Mbofu na kuibomoa yote na kisha kupinduka na watu 10 kufa papo hapo.
No comments:
Post a Comment