25 April, 2014

MJENGO WA LULU WATUMIKA KWA UTAPELI


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 Mjengo wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam umeingia kwenye lawama kufuatia madai kwamba, unatumika kwa kutapeli watu wanaotaka kununua nyumba maeneo hayo.
Mjengo wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kinasema nyumba hiyo baadhi ya watu wanaojiita madalali wamekuwa wakiwapeleka wateja kwa siri kwenye nyumba hiyo ambayo haijaisha na kusema inauzwa na Lulu mwenyewe.
“Baadhi ya madalali feki wamekuwa wakiwaleta wateja wanaotaka kununua nyumba maeneo haya. Wakifika wanasema Lulu anaiuza, wakiwa wameshaiona wanatoa fedha za usumbufu au za kuwapoza wasipeleke watej wengine na kutoa namba feki ya Lulu ili mteja ampigie.
“Wapo wateja walishanifuata na kusema wanampigia Lulu hapatikani, lakini waliponionesha namba yenyewe si ya Lulu.

“Siku moja mteja mmoja aliletwa na dalali kuiona nyumba, akaipenda, akampa dalali shilingi 300,000 za kumfanya asipeleke wateja wengine, akampigia Lulu hakupatikana. Alipokuja kwangu nikaiangalia namba hiyo ilisajiliwa kwa jina la Mwanahamis nani sijui,” kilisema chanzo hicho.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapaparazi walijifanya wateja wa kuinunua nyumba hiyo na kwenda kukutana na watu wawili waliodaiwa kuwa ndiyo madalali, Kitwana na Mambeze ‘Mchopa’.

Baada ya mazungumzo, madalali hao walidai kuwa, funguo za kuingia ndani ya nyumba hiyo anazo mama Lulu (Lucresia Karugila) na alisema angefika siku hiyo saa kumi jioni na kuwataka mapaparazi kurudi muda huo.
Wakati mapaparazi wetu wanaondoka, dalali mmoja alisema: “Nyie kama mmekuja kututega mmeliwa wenyewe, hapa hakuna mtoto wa kijijini. Wanaokuja hapa kutaka nyumba wanajulikana, nyie mmetumwa.”

Sosi mwingine alisema hivi karibuni alimuona Lulu akifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia nyumba hiyo ambayo imesimama ujenzi lakini hakuweka wazi kama alikuwa na nia ya kuiuza!

“Mimi mara ya mwisho nilimuona Lulu eneo hili na gari lake, naona alikuja kuangalia nyumba inaendeleaje na usalama pia. Mambo ya kuwa anaiuza hata siyajui ingawa kweli hata mimi nimekuwa nikiwaona watu wakija,” alisema sosi huyo ambaye hakutaka kutajaa jina lake.

Juzi, paparazi alipo msaka Lulu kwa njia ya simu kwa ajili ya kumuuliza kuhusu suala hilo ambapo, awali aling’aka, akasema: “Wewe ndiyo unaniambia kusema ukweli, sijui chochote. Naomba mnipe habari kwa upana ilivyo maana nyie waandishi mara nyingi mnakuaga wa kwanza kujua habari kuliko mhusika.”
 
Credit: GPL

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...