28 April, 2014

UJUMBE WA KUMTISHIA MAISHA MZEE WA UPAKO

 
 Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’akisisitiza jambo
 
SIKU chache baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Mhando kunusurika kutekwa, ujumbe wa tishio la kuuawa kwa Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Maombezi, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ umesambazwa.

Ujumbe huo ambao ulitumwa na mtu aliyejitambulisha kama msamaria mwema, ulisambazwa kwa watu mbalimbali na unaeleza kwamba mbaya wa Rose Mhando ana mpango wa kumuua Mzee wa Upako.

Uliendelea kufafanua kwamba sababu za kuuawa kwa mtumishi huyo wa Mungu ni kwa vile ameonekana kujipendekeza kumsaidia Rose baada ya tukio lake.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo, alisema kwa sasa kanisa lao lipo kwenye maombi maalumu kwa ajili ya kumuombea kiongozi wao ili Mungu amuepushe na hila zote za maadui.
“Hawana uwezo wa kumuua mchungaji wetu maana amefunikwa na damu ya Yesu,”alisema muumini wa kanisa hilo.
Waandishi wa habari hii walifunga safari mpaka kanisani kwa Mzee wa Upako na kufanikiwa kuzungumza na msaidizi wa mchungaji huyo ambaye hakutaka jina lake kuanikwa, alikiri kusikia madai hayo, lakini akasema hawayaamini.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...