08 May, 2014

SIMULIZI YA AUNT EZEKIEL: ILIKUWA AOLEWE AKIWA MDOGO, AKATOROKA NYUMBANI KWAO!


Aunt Ezekiel.
Anaitwa Aunt Ezekiel Grayson, si jina geni kwa wadau mbalimbali wa burudani nchini. Ni mrembo ambaye amepata jina kubwa kupitia sanaa yake ya uigizaji wa filamu aliyoianza miaka saba iliyopita.
Msanii huyo ambaye ni mtoto wa damu wa aliyekuwa mchezaji mahiri wa Simba Sports Club ‘Wekundu wa Msimbazi’ marehemu  Ezekiel Grayson.
Aunt Ezekiel amepitia maisha  magumu sana kabla
 ya kufika alipo leo. Ili kujua maisha yake halisi fuatilia hapa.....
Mwandishi:  Mambo Aunt? Natumaini uko mzima. Mimi ningependa kujua zaidi historia ya maisha yako kuanzia ulikotokea hadi ulipo sasa.
Aunt: Duu! Sawasawa! Mimi nimezaliwa  mwaka 1988 hapahapa jijini Dar es Salaam. Ni mtoto wa pili kwa mama yangu mzazi kwa sababu kwa  baba  nina ndugu zangu wengine.
Mwandishi: Kwa hiyo una maanisha kabla ya baba yako kuwa na mama yako alikuwa na mwanamke mwingine?
Aunt: Ndiyo.
Mwandishi: Wakati huo ulikuwa ukiishi hapa Dar es Salaam sehemu gani?
Aunt: Nilikuwa nikiishi Ilala  na nilipata elimu yangu ya msingi katika Shule ya Msingi Bunge mwaka 1995 mpaka 1998, nikaenda kumalizia Kisarawe, Pwani.
Mwandishi: Kwa nini ulikwenda kumalizia huko? Ilikuwa bording (shule ya bweni)?
Aunt: Hapana, baba yangu alipata matatizo akapelekwa jela hivyo kukawa hakuna mtu wa kunilipia ada pale Shule ya Bunge, hivyo wakanipeleka kule kwa babu na bibi yangu.
Mwandishi: Mama yako alikuwa wapi kipindi hicho?
Aunt: Mama yangu alifariki dunia mwaka 1995, hivyo nilibaki na baba na ndugu zangu wengine.
Mwandishi: Sasa hukuona kama kuna tofauti wakati ulikuwa umeshazoea maisha ya mjini?
Aunt: Tofauti ilikuwepo kubwa sana lakini ilibidi nizoee niweze kusoma tu maana sikuwa na jinsi.
Mwandishi: Ilikuwaje baada ya kumaliza shule, uliendelea kuishi Kisarawe?
Aunt: Yaani maisha yalizidi kuwa magumu sana, niliendelea kukaa huko lakini baadaye ilibidi nitoroke.
Mwandishi: Kwa nini ulitoroka, ulikuwa ukiteswa?
Aunt: Hapana, nilipomaliza tu shule kuna mwanaume alikuja kwa babu akasema anataka kunioa.
“Sikuwa tayari kabisa lakini kwa vile alikuwa na pesa ndugu zangu waliona bora niolewe naye kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kunisomesha tena.
“Ilibidi nitoroke, nikaja Gongo la Mboto (Dar es Salaam). Kuna sehemu inaitwa Mazizini.
“Nilisema nije nitafute kazi yoyote ile, popote pale ili niweze kujinusuru na kuolewa nikiwa katika umri mdogo.
Aunt Ezekiel ametoroka nyumbani Kisarawe na kukimbilia Dar kutafuta kazi.
Endelea kutembelea JoJoTheFighter ili kujua nini kiliendelea baada ya Aunt toroka nyumbani na kukimbilia mjini
 
Credit: Imelda Mtema Via G.P.L

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...