29 May, 2014

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI INGAWA ZINASIKITISHA LAKINI HUNA BUDI KUPITIA HAPA NA KUTOA MSAADA WA KUMSAIDIA BI MWANAIDI VUAI SALEH ALIYEUNGUA KWA MAJI YA MOTO

 Bi Mwanaid Vuai Saleh akiwa ameathirika kiasi hicho kama anavyoonekanav pichani akiwa katika hospitali ya Jeshi Bububu Unguja akiendelea na Matibabu yake akisubiri misaada ya Wasamaria wema ili kupata kusafirishwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi ili kurudisha hali yake kiafya.
Kwa  sasa amepata baraka zote kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar kupata missada kama inavyosomeka hapo chini. 

Kumradhini kwa kuweka picha hii ya Bi Mwanaid Vuai Saleh, kwa maadali ya habari haifai.

Aliyepata ajali hiyo ya  kuanguka wakati akiwa katika kazi zake za nyumbani na kuanguka katika sufuria la maji ya moto baada ya kuona kizunguzungu na kuangukia humo na kumuathiri kiasi hicho na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Jeshi Bububu akipata matibabu ya majaraha hayo.
Bi Mwanaid Vuai ni Mkaaza wa Shehia ya Chumbuni Wilaya ya Mjini Unguja 
Anaomba msaada wa Fedha ili kusafirishwa nje ya Nchi kupelekwa India kwav matibabu  zaidi 
Kwa kila Mwananchi atakayepata fursa ya kumsaidi Bi Mwanaid Vuai, ili kupata matibabu, anaombwa kuwasiliana na Mdau wa Blog hii, kwa Namba  0777424152.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...