
Taarifa mpya ni kwamba Emmanuel Mbasha anayekabiliwa na kesi ya kumbaka mdogo wa mke wake, ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti katika mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Kwenye masharti aliyotimiza Emmanuel ambae ni mume wa mwimbaji Flora Mbasha, ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili ambao wote ni wafanyakazi katika taasisi inayotambulika kisheria.
June 17 2014 mbele ya hakimu Willbaforce Rwago wa mahakama hiyo, mwendesha mashtaka wa serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshatakiwa alitenda kosa hilo Mei 23 mwaka huu eneo la Tabata Kimanga.
Emmanuel Mbasha alifikishwa mahakamani hapo na kukana shitaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 anaedaiwa kuwa shemeji yake hivyo akarudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Mwendesha mashtaka wa serikali alieleza Mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na imepangwa kutajwa tena July 17 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment