"Mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako.
Mchungaji, naomba uelewe kuwa
nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni
kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango
kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa
kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi
kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!
Mnamo
tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la
mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu
aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI
FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa
na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti
maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!
Nashukuru
kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa
kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri
ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??
Pia
napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa
taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa
na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao
wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na
aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna
nini hapo??
Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!
Binafsi
nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika
mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli
ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest
hill!!
Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano
wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi
uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es
salaam!!
Lakini uliniomba mkewangu abaki na
wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako
kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu
nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako
alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!
Kwaa
taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale
hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa
chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala
wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera
hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata
namba ya dereva taxi ninayo!!
Yote haya
nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini
nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa
yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii
sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa
unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga
kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point
hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu
jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa
kunitishia jela miaka 30!!!
Wewe ni mpuuzi na
shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa
NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the
end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!
Bila
kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta
ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya
ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki
je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa
wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba
ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni
mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku
wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea
Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda
Yes
nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu
kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa
mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako
ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana
na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa
muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma,
kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!
Mkewangu,
kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui
kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye
nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!
Lakini
nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe
tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini
kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe
Hivi
kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili
wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata
mkewangu??
Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi
kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae
jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu
kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto
wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia
sana!
Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni
impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini
tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri
ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!
Kumbuka
hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki
wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa
dhambi hii!!
Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda
katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini
mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!
Mwisho
nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia
kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye
pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali
kwenye ukoo!!
Nakuonya tena kwa mara nyingine,
muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na
wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!
Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya
watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya
kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha
kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe
ni nyoka!!
Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa
familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala
connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi
nimepiga magoti!
Nitapambana na wewe mpaka
mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue
kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo
kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya
umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."
CREDIT: WANABIDII
No comments:
Post a Comment