Kibonde wa Clouds anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii
eneo la Makumbusho, amemgonga dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki
walipofika kupima ajali, Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake
kasepa! Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia. Walifanikiwa
kumkamata eneo la Mwenge. Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba
arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde
kagoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake, trafiki naye kagoma
kushuka. Mchezo ulioendelea Kibonde aliondoa gari na kuanza kupiga
misele, akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo! Trafiki aliwasiliana na
wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila kiunga cha
jiji hususani eneo la Mwenge na Ubungo. Hayawi, hayawi yakawa, Kibonde
akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo nikashuhudia senema ya Kibonde
na trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya
Kibonde iliyokuwa kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za kupunguza
mwendo. Trafiki alikomaa kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria kumtaka
Kibonde asimame huku akipaza sauti ktk radio call akisema ananigonga,
afande, ananigonga! Akiwa ktk hali hiyo, kuna gari ilikotokea sikujua
ikakatisha kati ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa kigingi cha
gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi
livutwe hadi polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa Oystabay! Kwa
utafiti mdogouliofanywa na shuhuda wa skendo hii,
ni kwamba Kibonde na watu wengine aliokuwanao ndani ya gari lake
walikuwa 'TINGASI'!
No comments:
Post a Comment