MASHOGA kutoka nchi tatu za Afrika Mashariki wamekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Taarifa
zilizopatikana jijini Dar es Salaam, zinasema mashoga hao walikutana
juzi katika Ukumbi wa Kivukoni 3 ulioko katika Hoteli ya Serena na
kuwashirikisha wasichana wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mashoga hao wapatao 50 walitoka katika nchi za Kenya na Uganda na waliungana na wenzao wa Tanzania.
Katika
kuhakikisha malengo ya mkutano huo hayatambuliki, katika ubao wa
matangazo wa hoteli hiyo waliutambulisha kama ulikuwa ni mkutano wa
kujadili masuala ya kimataifa ya afya ulioitwa International Health
(SA).
Mwandishi
wetu aliyepata taarifa za uwepo wa mkutano huo, alishuhudia jinsi
mkutano huo ulivyokuwa ukiendeshwa kwa usiri wa hali ya juu kwa kuwa
kila aliyekuwa akitaka kuingia ukumbini alikuwa akizuiwa.
Pamoja
na watu wasiohusika kutotakiwa kuingia ukumbini, hata wahudumu wa
hoteli hiyo walikuwa wakiruhusiwa kuingia ukumbini kwa tahadhari ili
wasijue kinachoendelea.
Katika
kuhakikisha hilo linafanikiwa, mashoga hao walikuwa wakisitisha mjadala
kila wahudumu walipokuwa wakiingia ukumbini kwa ajili ya kutoa huduma
na mazungumzo yalikuwa yakiendelea baada ya wahudumu kutoka ukumbini.
Pamoja
na ulinzi uliokuwa mahali hapo, taarifa zilisema mada kuu
iliyowakutanisha mashoga hao ilikuwa ni kujadili changamoto
zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi. Pia taarifa zinasema
walikuwa wakijadili namna ya kufanya utafiti wa kukabiliana na
changamoto hizo.
Pamoja
na mashoga hao kuonyesha walikuwa wakijadili masuala ya afya ya
kimataifa, Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris
Mwamwaja, alisema wizara hiyo haikuwa na taarifa za mkutano huo.
Kwa
mujibu wa sheria za Tanzania ushoga hauruhusiwi lakini wiki iliyopita
Mahakama ya Kikatiba nchini Uganda ilifutilia mbali sheria dhidi ya
wapenzi wa jinsia moja, ambayo ilisababisha mataifa kadhaa ya magharibi
kuinyima misaada.
Sheria
hiyo ilizua mjadala si tu nchini Uganda bali kote duniani kiasi cha
kuyafanya mataifa ya magharibi yalazimike kuingilia kati.
Mahakama
ilisema muswada uliopitishwa kabla ya kuidhinishwa na rais kuwa sheria,
ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kuupitisha na kwa
hivyo ulikuwa kinyume na sheria.
Sheria
hiyo iliharamisha hatua zozote za kueneza au kushawishi mapenzi ya
jinsia moja na wakati huo huo ikiwajumuisha wanawake wasagaji katika
kundi hilo.
Wabunge
nchini Uganda huenda wakalirudisha upya bungeni suala hilo, mchakato
unaotarajia kuwa mrefu ukizingatia sheria ya sasa ilichukua miaka minne
hadi kupitishwa.