05 August, 2014

UGANDA YAFUTA SHERIA ILIYOPINGA USHOGA!

Waganda wakiwa wanapinga uwepo wa ushoga katika taifa lao
Korti ya kikatiba nchini Uganda imefuta sheria dhidi ya mashoga iliyotiliwa saini na Rais Yoweri Kaguta Museveni Februari mwaka 2014, ikibaini kwamba wabunge waliyoidhinisha sheria hiyo hawakutimiza idadi iliyokua inahitajika.
“ Sheria dhidi ya ushoga imefutwa na haina nguvu tena kwa kuwaadhibu mashoga”, amesema mkuu wa korti ya kikatiba.

Sheria hiyo imekua imepiga marufuku mapenzi ya watu wa jinsia moja na kuwataka raia kuwafichua watu wote wanaojihusisha na kitendo hicho cha ushoga. Adhabu ya kifungo cha maisha jela ilikua inamkabili mtu anaye jihusisha na ushoga, adhabu ambayo ililalamikiwa na jumuiya ya kimataifa. Hiyo sheria iliwafanya wafadhili wengi wa Uganda kuifutia serekali ya nchi hiyo baadhi ya misaada waliyokua wakiipa.
Wanaharakati wa haki za mashoga wakipinga sheria dhidi ya ushoga Uganda
Kufutwa kwa sheria hiyo kumepongezwa sana  na wanaharakati wa haki za mashoga nchini Uganda,

“ Sheria dhidi ya ushoga kwa sasa haina kazi tena”,  hayo yalisemwa na Andrew Mwenda, ambaye ni mwanahabari akiwa pia mwanaharakati wa kuitetea mashoga.

Wanaharakati wa haki za mashoga wapongeza kufutwa kwa sheria dhidi ya ushoga UgandaKassisi Martin Ssempa, anaepinga ushoga, amesema Marekani itasababisha Uganda ikumbwe na laana kama ile ya Sodoma na Gomora, akilani vikwazo viliyochukuliwa na Marekani dhidi ya Uganda kufuatia kupitisha sheria dhidi ya ushoga.

Kasisi huyo, akivalia joho amefanya ibada ya dakika chache ndani ya korti kulikokua kumejaa watu wakisubiri uamzi wa majaji, ili kutaka majaji wasifute sheria hiyo.

Chanzo: RFI 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...