26 September, 2014

AIBU! MREMBO ASABABISHA STEVE NYERERE KUZOMEWA UWANJANI




NYOTA wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki wa Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa ‘kihasarahasara’.Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’akiwa na mrembo huyo.Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20, 2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya Yanga na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji walishinda 2-0.
Steve alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani (zinazotumiwa na Yanga).
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo walipozomewa na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa kuwa, demu huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara hadharani

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...